Saturday, June 23, 2012

KESI YA EPA KUANZA KUSIKILIZWA


KESI YA WIZI WA SH 6 BILIONI ZA AKAUNTI YA MADENI YA NJE (EPA) YA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT), INAYOWAKABILI WASHTAKIWA WATANO IMEPANGWA KUSIKILIZWA MFULULIZO.  HAKIMU ALOYCE KATEMANA WA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU, ALIELEZA HAYO JANA ALIPOKUWA AKIAHIRISHA KESI HIYO ILIPOTAJWA MAHAKAMANI HAPO INAYOWAKABILI BAHATI MAHENGE, MANASE MWAKALE, DAVIES KAMUNGU, GODFREY MOSHA NA EDDAH MWAKALE.

HAKIMU KATEMANA ALIIAHIRISHA KESI HIYO HADI JULAI 13, KWA AJILI YA KUENDELEA KUSIKILIZWA.  WASHTAKIWA HAO WANATARAJWA KUENDELEA KUJITETEA DHIDI YA MASHITAKA YANAYOWAKABILI BAADA YA MAHAKAMA KUWAONA KUWA WANA KESI YA KUJIBU.  MAHENGE NA WENZAKE KWA PAMOJA WANADAIWA KUWA KATI YA MWAKA 2003 NA 2005 WALIKULA NJAMA YA KUIIBIA BENKI KUU YA TANZANIA, SH 6,041,899,876.45 BAADA YA KUDANGANYA KUWA KAMPUNI YAO YA CHANGANYIKENI ILIPEWA DENI NA KAMPUNI YA MARUBENI YA NCHINI JAPAN. 

No comments:

Post a Comment