"MLIPUAJI WA KUJITOA MUHANGA ALIKUWA AKIJARIBU
KUENDESHA BASI DOGO LILILOJAA MABOMU NA KUWAPITA WALINZI, LAKINI WALIMLAZIMISHA
KUSIMAMA KABLA YA KUMFYATULIA RISASI. NA GHAFLA AKALIPUKA NA ASKARI WAWILI
WALIUAWA NA RAIA WATATU KUJERUHIWA," AFISA USALAMA MOHAMED LIBAN ALIIAMBIA
AFP.

"SHAMBULIO HILO LILIZIMWA KWA VILE MLIPUAJI BOMU
HAKUMUDU KUINGIA KAMBINI," ALISEMA.
KAMBI YA KIJESHI YA AFGOYE IKO KAMA KILOMITA 30 KUTOKA
MOGADISHU.
MSEMAJI WA AL-SHABAAB SHEIKH ALI MOHAMUD RAGE ALIDAI
KUHUSIKA NA SHAMBULIO HILO KATIKA TAARIFA YA REDIO ANDALUSI INYOWAUNGA MKONO
AL-SHABAAB, NA KUTISHIA MASHAMBULIZI ZAIDI HUKO AFGOYE, KWA MUJIBU WA MTANDAO
WA HABARI WA KULMIYE NEWS NETWORK WA SOMALIA.
MAJESHI YA SOMALIA NA UMOJA WA AFRIKA HIVI KARIBUNI
YALIUTEKA MJI WA AFGOYE KUTOKA UDHIBITI WA AL-SHABAAB. RAISI WA SOMALIA SHEIKH
SHARIF SHEIKH AHMED ALIITEMBELEA AFGOYE MAPEMA WIKI HII ILI KUKUTANA NA MAAFISA
WA ENEO HILO, VIONGOZI WA KIKABILA NA WA KIDINI NA KUJADILIANA NAO NJIA ZA
KUIMARISHA USALAMA NA KUHAKIKISHA USALAMA WA RAIA.
No comments:
Post a Comment