Monday, June 18, 2012

GODFREY ZAMBI AINGIA MATATANI


MBUNGE WA MBOZI MASHARIKI, GODFREY ZAMBI (CCM), AMEINGIA MATATANI BAADA YA KAMPUNI MOJA YA UNUNUZI WA KAHAWA KUMSHTAKI MAHAKAMANI IKIMDAI FIDIA YA SH2.4 BILIONI.
KWA MUJIBU WA HATI YA MADAI ILIYOWASILISHWA KORTINI NA MKURUGENZI NA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA LIMA LTD, ERIC NG’MARYO, ZAMBI AMEWASABABISHIA HASARA YA SH1.8 BILIONI KUTOKANA NA MATAMSHI YA KUIKASHIFU.
 “MDAIWA AMEANZISHA KAMPENI ZA KUCHAFUA KAMPUNI YETU ILI KUUA USHINDANI ILI VIKUNDI VYA WAKULIMA ANAVYODAI KUVIWAKILISHA VISIWEZE KUPATA USHINDANI,” AMEDAI NG’MARYO.
MSINGI WA KESI HIYO NI MAKALA YALIYOCHAPWA KATIKA GAZETI MOJA CHINI YA KICHWA CHA HABARI “MBUNGE CCM APINGA UTEUZI WA JK”.
KATIKA MAKALA HAYO, ZAMBI AMEKARIRIWA AKIPINGA UTEUZI WA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA KAHAWA TANZANIA (TCB), DK EVE HAWA SINARE NA BAADHI YA WAJUMBE WA BODI HIYO. NG’MARYO PIA NI MMOJA WA WAJUMBE WA BODI HIYO YA WAKURUGENZI.
KUPITIA TAARIFA HIYO, MBUNGE HUYO ANADAIWA KUITUHUMU KAMPUNI YA LIMA LTD YENYE MAKAO YAKE MJINI MOSHI KUSHAWISHI WAKULIMA KUUZA KAHAWA MBIVU KWA BEI NDOGO.
“UHALISIA NA TAFSIRI YA KAWAIDA YA KAULI HIYO YA ZAMBI NI KWAMBA LIMA LTD NI WALANGUZI WANAOPATA FAIDA KUBWA KWA KUWANYONYA WAKULIMA WA KAHAWA,” AMELALAMIKA NG’MARYO.
KATIKA KUTHIBITISHA UHALALI WA FIDIA HIYO, KAMPUNI YA LIMA LTD ITAEGEMEA USHAHIDI KUWA ZAMBI NI MBUNGE ANAYETUMIA NAFASI YAKE KUANZISHA VITA BINAFSI NA KAMPUNI HIYO.
 “ZAMBI NI MBUNGE WA BUNGE LA JAMHURI, LAKINI ANAFANYA MAMBO KINYUME NA SHERIA ZA NCHI ANAZOPASWA KUZILINDA ZIKIWAMO KANUNI ZINAZOSIMAMIA SEKTA YA KAHAWA,” AMEDAI.
KAMPUNI HIYO INAIOMBA MAHAKAMA KUMWAMURU MBUNGE HUYO AWALIPE SH2.4 BILIONI, KAMA FIDIA NA IWE FUNDISHO KWA WENGINE.
PIA KAMPUNI HIYO INAIOMBA MAHAKAMA KUU KUTOA ZUIO DHIDI YA MBUNGE HUYO KUENDELEA KUCHAPISHA TAARIFA ZA KUIKASHIFU KAMPUNI HIYO.
ZAMBI ALIPOULIZWA ALISEMA HAJAPATA TAARIFA YA KUSHTAKIWA, LAKINI KAMA ATAARIFIWA RASMI NA MAHAKAMA, ATAKAA NA WANASHERIA WAKE KUJUA NINI CHA KUFANYA.
KESI HIYO ILIYOFUNGULIWA JUMATAN

No comments:

Post a Comment