Sunday, June 17, 2012

MAASKOFU WAPINGA KIPENGELE...................


BARAZA LA MAASKOFU WAKUU WA MAKANISA YA KIPETEKOSTE TANZANIA (PCT)WAMETOA TAMKO LINALOITAKA SERIKALI KUTOWEKA MASUALA YA KIDINI, UKABILA NA MAMBO YOTE YANAYOHUSU UBAGUZI WA NAMNA YOYOTE WAKATI ITAKAPOTEKELEZA SUALA LA  SENSA YA WATU NA MAKAZI INAYOTARAJIA KUFANYIKA MWAKA HUU.
PIA MAASKOFU HAO WAMEITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA ZINAZOSTAHILI IKIWA NI PAMOJA NA KUSHUGHULIKIA VYANZO VYA VURUGU ZILIZOTOKEA MEI 28 MWAKA HUU VISIWANI ZANZIBAR AMBAZO ZILISABABISHA KUCHOMWA KWA MAKANISA NA VITABU VYA BIBLIA NA TENZI ZA ROHONI.
TAMKOA LA MAASKOFU HAO LILISOMWA UPANGA  JIJINI DAR ES SALAAM JANA NA MAKAMU  MWENYEKITI WA BARAZA HILO TAIFA   ASKOFU DANIEL  AWETI KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI.
AKIZUNGUMZIA SUALA LA SENSA ALISEMA NI HATARI KUHUSISHA MASUALA YA DINI, MADHEHEBU YA WATU,IMANI,UKABILA KWA KUWA MASUALA HAYO HAYANA MSINGI WOWOTE NA YANAWEZA KUCHOCHEA MGAWANYIKO KATIKA JAMII.
“SENSA YA WATU NA MAKAZI NI MUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU,HUTUWEZESHA KUPATA TAKWIMU ZINAZOSAIDIA SERIKALI KUPANGA MIPANGO YA MAENDELEO KWA KUZINGATIA MGAWANYO BORA WA RASIMALI TULIZONAZO”ALISEMA AWETI NA KUONGEZA;
“SISI TUNAOIMBA SERIKALI KUTOWEKA MASWALI YENYE LENGO LA KUTAKA KUJUA DINI, DHEHEBU, AU IMANI YA MTU AU KABILA LA MTU,MASWALI YA NAMNA HII HAYAFAI NA HAYANA FAIDA WALA TIJA KWA TAIFA LETU NA ZAIDI YANAWEZA KUCHOCHEA MGAWANYIKO KATIKA JAMII”ALISEMA HUKU AKISISITIZA KUWA WATANZANIA HATUPASWI KUTAMBUANA KWA DINI WALA KABILA ZETU.

ALISEMA MAKANISA HAYO KWA PAMOJA WAMEKUBALIANA KUHAMASISHA WAUMINI WAO NA WANANCHI KWA UJUMLA UMUHIMU WA KUSHIRIKI KATIKA SENSA ILI KUSAIDIA KUHARAKISHA MAENDELEO YA NCHI.

No comments:

Post a Comment