Sunday, June 17, 2012

SIMANJIRO WAMETISHIA KUHAMIA CHADEMA


BAADHI YA WENYEVITI WA SERIKALI ZA VIJIJI, VIONGOZI WA KIMILA(MALWAIGANANI),WAJUMBE WA SERIKALI ZA VIJIJI  SANJARI NA VIONGOZI WA CCM WILAYANI SIMANJIRO WAMETISHIA KUHAMIA CHADEMA ENDAPO SERIKALI IKISHINDWA KUWARUDISHIA ENEO LA EKARI 2000 WANAYODAI KUPORWA NA MWENYEKITI WA CCM WILAYANI HUMO,BROWN OLE SUYE.
WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JANA VIONGOZI HAO  ZAIDI YA 100 AMBAO WAMEFUNGA SAFARI YA KUTOKA WILAYANI SIMANJIRO HADI JIJINI ARUSHA  PIA WALIMTAKA RAIS JAKAYA KIKWETE KUINGILIA KATI MGOGORO HUO KWA KUWA WANANCHI WILAYANI HUMO WAMEPOTEZA IMANI YA SERIKALI YAO.
OLAMAYAN OLE LANGAA,AMBAYE NI MZEE WA MILA WILAYANI HUMO MAARUFU KAMA LAIGWANANI ALISEMA KWAMBA YEYE KAMA KADA WA CCM NA KIONGOZI WA KIMILA WILAYANI  HUMO AMECHOKA KUONA WANANCHI WAKINYANYASWA KWENYE ARDHI YAO.
ALISEMA KWAMBA AMEPOTEZA IMANI NA SERIKALI YA CHAMA TAWALA KWA KUMKUMBATIA MWENYEKITI WA CCM WILAYANI HUMO,OLE SUYE AMBAYE ALIMTUHUMU KWAMBA AMEPORA ARDHI YA EKARI 2000 KATIKA ENEO LA LEBOSOIT.
“WANANCHI TUMEPOTEZA IMANI NA SERIKALI YA CCM HAIWEZEKANI  KIONGOZI WA CHAMA AMBAYE TUNAMTEGEMA APORE ARDHI YETU KUBWA KIASI HIKI”ALISEMA OLE LANGAA

No comments:

Post a Comment