Friday, June 22, 2012

HUKU MADAKTARI HUKU WAALIMU


BERNARD KOMBA
BEN KOMBA/PWANI-TANZANIA/6/22/2012 8:30:29 AM
CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA KIBAHA KWA HALMASHAURI ZA MJI NA WILAYA, KIMETANGAZA MGOGORO WA WA SIKU 30 NA SERIKALI IKIWA NI NJIA MOJAWAPO YA KUISHINIKIZA SERIKALI KULIPA MADAI YAO IKIWA SEHEMU YA KUUNGA MKONO HATUA ILIYOCHUKULIWA NA CWT TAIFA.
AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA PAMOJA NA WALIMU KATIKA SHULE YA MSINGI MLANDIZI, KATIBU WA CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA KIBAHA, BIBI. ELIZABETH THOMAS AMESEMA MGOGORO HUO SIO MGOMO ILA NI TAHADHARI AMBAYOM IPO KISHERIA KABLA YA MGOMO.
BIBI. THOMAS AMEFAFANUA BAADA YA SIKU 30 KUPITA BILA ERIKALI KUSHUGHULIKIA MADAI YAO, WATATOA TENA SAA 48 NAZO ZIKIPITA BILA HATUA YOYOTE KUCHUKULIWA HAPO NDIPO ITAKAPOPIGWA KURA NA WANACHAMA WOTE NA IKIZIDI HATA KURA MOJA MGOMO HUO UTAKUWA HALALI NA ZOEZI LA UPIGAJI KURA LITAKUWA TAREHE 9 NA 10 JULAI.
KATIBU HUYO BIBI. ELIZABETH THOMAS AMEONGEZA KUWA HATUA HIYO INAFUATIA SERIKALI KUWA KICHWA NGUMU KATIKA KUSIKILIZA MADAI MBALIMBALI YA WALIMU ILI HALI IKITOA KIPAUMBELE KATIKA SEKTA NYINGINE NA KUWAACHA WALIMU DHOOFU KIHALI, NA KWA KUTUMIA SHERIA ZILIZOPO NAO WAMEAMUA KUANZISHA MGOGORO WA KIMASLAHI NA SI VINGINEVYO NA BILA SHINIKIZO KUTOKA KOKOTE.
AKITOA TAMKO KUHUSIANA NA HATUA AMBAYO IMECHUKULIWA NA CHAMA CHA WALIMU TAIFA, MWENYEKITI WA CWT WILAYA YA KIBAHA BW. RAJABU NGAMBAGE AMETANGAZA RASMI KUUNGA MKONO MGOGORO HUO ULIOANZA TAREHE 8 JUNI NA UNATAZAMIWA KUISHA JULAI 5 NA KAMA KUTAKUWA HAKUNA KILICHOFANYIKA JULAI 9 MPAKA 10 WATAPIGA KURA KUIDHINISHA KUFANYIKA KWA MGOMO.

No comments:

Post a Comment