Tuesday, June 19, 2012

AJALI YAUWA KILIMANJARO


AJALI ZA BARABARANI ZIMEENDELEA KUUTIKISA MKOA WA KILIMANJARO, JANA BASI DOGO LA ABIRIA LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATANO PAPO HAPO NA KUJERUHI 13.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA KILIMANJARO, RAMADHAN NG’AZI, ALISEMA AJALI HIYO ILITOKEA JUZI SAA 1:00  USIKU WAKATI BASI HILO LIKITOKEA KIJIJI CHA NG’UNI KWENDA BOMANG’OMBE, KUPITIA KWARE WILAYANI HAI.
AJALI HIYO ILITOKEA ENEO LA MBOSHO, KATA YA MASAMA, BAADA YA DEREVA WA BASI HILO DOGO AINA YA TOYOTA HIACE NAMBA T179  AAX AMBAYE HAJAFAHAMIKA, KUSHINDWA KUDHIBITI GARI HILO.
NG’AZI ALISEMA WALIOKUFA WAMETAMBULIWA KUWA NI ELINAWENGA LEAMA (90) MKAZI WA ISUKA, FRED JACKSON (23) MKAZI WA MASAMA NA RAPHAEL KIMARO(55) MKAZI WA NG’UNI.
WENGINE WALIOKUFA NI RICHARD MUNUO (55) MKAZI WA KIJIJI CHA NG’UNI NA BARAKA NG’OKO (45), AMBAYE NI MKAZI WA ARUSHA.
WALIOJERUHIWA NA UMRI WAO UKIWA KWENYE MABANO, NI OSCAR SIAO (40-45), ALISENDA SIRAEL (50), LEONARD MUNISI (32), HUSSEIN ABDI (63), AMINADABU MUNUO(6) NA RICHARD ARNOLD (18).
WENGINE WALIOJERUHIWA NI DAVID JOSHUA (39), NOEL ONESMO (25), MARRY WITNESS (44), WALTER TARIMO (37), ONISAEL ANANKYA (70), HELEA NGUNDA (60) NA WILINANDA AMOSI (37).
ALISEMA MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA CHUMBA CHA KUHIFADHI MAITI CHA HOSPITALI YA KIBONG’OTO ,WAKATI MAJERUHI WALIPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA YA KCMC KWA MATIBABU.
KAIMU KAMANDA HUYO ALISEMA INGAWA UCHUNGUZI WA CHANZO CHA AJALI HIYO UNAENDELEA, LAKINI INAONYESHA MWENDOKASI UMECHANGIA KWA KIWANGO KIKUBWA.

No comments:

Post a Comment