Tuesday, May 22, 2012

MUUAJI WA TERREBLANCHE MATATANI


Polisi wa Afrika Kusini
Mmoja kati ya wanaume wawili walioshtakiwa kwa kumuua Eugene Terreblanche mwaka 2010 amepatikana na hatia.
Chris Mahlangu, alipatikana na hatia ya mauaji ingawa mshtakiwa mwenzake Patrick Ndlovu, aliachiliwa kwani alikuwa na miaka kumi na tanao wakati wa kitendo hicho.
Polisi waliimarisha doria hiikatika mji wa Ventersdorp, nchini Afrika Kusini wakati hukumu ikisubiriwa kwa vijana hao wawili wa Kiafrika waliotuhumiwa kumuua Eugene Terre' Blanche miaka miwili iliyopita.
Bwana Terre' blance alikuwa kiongozi wa mrengo wa kulia wa vuguvugu la kupigania utawala wa kizungu la Afrikaan Resistance Movement.
Wanaharakati wengi wa kutoka vuguvugu walipiga kambi nje ya mahakama hiyo wakiwa wamevalia sare za chama hicho na wamebeba bunduki.
Wawili hao walikanusha mashtaka ya kumuua muajiri wao na kutekeleza uwizi wa mabavu.
Mahlangu anadai kuwa alikuwa akijitetea ili hali mvulana anayeshtakiwa pamoja naye amekanusha kuhusika na uhalifu huo.
Kizingiti kikubwa katika kesi hii ni kuwa Mahlangu na mvulana huyo walikataa kutoa ushahidi wao, wakati wa kesi hiyo.
Hali ya wasi wasi ilitanda nje ya makahakama hiyo kama ilivyokuwa wakati wa kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo miaka miwili iliyopita.
Eugene Terreblance
Wakati huo, polisi walikabiliwa na wakati mgumu kuwatenganisha makundi ya wafuasi wa pande hizo mbili.
Lakini idara ya polisi na chama cha AWB zimesema kuwa ghasia zozote hazitarajiwi.
Polisi wamesema ikiwa mambo yatakwenda kinyume na matarajio yao, imeweka mikakati thabiti ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote atakayevuruga shughuli za mahakama.
Mwezi uliopita, wakati mawakili walipokuwa wakitoa tetesi zao za mwisho mbele ya mahakama hiyo, jaji alionya kuwa hukumu huenda ikachukua muda mrefu lakini haijulikani, ikiwa uamuzi huo utachukua zaidi ya siku moja kutolewa.
Hata hivyo pande zote zinatarajiwa kukata rufaa baada ya hukumu kutolewa.

No comments:

Post a Comment