Tuesday, May 22, 2012

Didier Drogba kuondoka Chelsea


Didier Drogba
Hatimaye athibitisha ataondoka Chelsea
Mshambulizi Didier Drogba ataihama timu ya Chelsea ya England msimu huu wa joto, baada ya kukichezea klabu kwa muda wa miaka 8.
Mchezaji huyo wa Ivory Coast, na mwenye umri wa miaka 34, alifunga bao la ushindi katika fainali ya mwaka huu ya Kombe la klabu Bingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern.
Drogba atakuwa huru kujiunga na klabu chochote kile, kwani mkataba wake na timu ya Blues unaelekea kumalizika.
Baada ya miezi mingi ya mashabiki kutojua hatma yake, Drogba amethibitisha sasa ataondoka Stamford Bridge.
"Nilitaka kukomesha hali hii ya shaka na kuthibitisha kwamba ninaondoka Chelsea", alielezea Drogba katika tovuti ya Chelsea.
"Umekuwa ni uamuzi mgumu sana kwangu, lakini ni fahari kwangu kwa ufanisi tulioweza kupata, lakini wakati umewadia kwa changamoto mpya", alielezea.
Aliongezea: "Kama timu, tumefanikiwa katika mengi, na tukishinda vikombe muhimu."
"Ningelipenda kuitumia nafasi hii kuwashukuru wote katika klabu, hasa Roman Abramovich na wachezaji wenzangu."
Tatizo la mkataba wa Drogba ulianza msimu uliopita, wakati klabu kilipokataa kumuongezea miaka miwili zaidi katika mkataba wake.
Wasiwasi wa mashabiki ulizidi wiki chache zilizopita, iwapo Drogba ataendelea kuichezea Chelsea, hasa baada ya timu yake kuibuka mshindi katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Liverpool, na pia alipofunga bao la kusawazisha Jumamosi, na vilevile kufunga goli la ushindi wakati wa mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Bayern.

No comments:

Post a Comment