Monday, December 26, 2011

UNYANYAPAA WA WANAWAKE KATIKA MAGARI HUKO OSRAEL

Mamia ya Wayahudi wanaofuata dini yao kiasilia, wamepambana na polisi karibu na Jerusalem kwa sababu ya mvutano kuhusu kuwatenga wanawake na wanaume.
Waisrail wanazozana kuhusu kuwatenga wanawake
Afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa katika mji wa Beit Shamesh, wakati polisi walipoitwa kuondoa ilani kwenye barabara kuu, inayoamrisha wanawake wajitenge na wanaume.
Makundi ya Wayahudi wanaofuata dini yao kiasili waliwafukuza polisi na kuwarushia mawe.
Ghasia hizo ndio za karibuni kabisa katika mfululizo wa matukio mengine nchini Israil, ambapo wanawake walilazimishwa kukaa nyuma kwenye mabasi, katika maeneo ya Wayahudi hao, ingawa mahakama yametoa amri kuwa wanaweza kukaa watakapo.

No comments:

Post a Comment