Monday, December 26, 2011

MAREHEMU WAKUMBUKWA NCHINI NIGERIA

Mamia ya watu wamehudhuria sala ya kuwakumbuka marehemu nchini Nigeria kwenye kanisa la Wakatoliki, ambamo watu zaidi ya 30 waliuwawa katika shambulio la mabomu Jumapili.
Nigeria, kanisa liloshambuliwa
Watu zaidi ya 40 walikufa.
Kikundi cha Kiislamu cha Boko Haram, kimesema kuwa kilifanya mashambulio hayo.
Kiongozi mkuu wa upinzani, Muhammadu Buhari, ameishutumu serikali kuwa imechelewa kuanza kushughulikia mashambulio hayo; na alisema Rais Goodluck Jonathan hakusema kitu, hadi mashambulio hayo kuanza kulaaniwa dunia nzima.

No comments:

Post a Comment