MWANZILISHI
WA WIKILEAKS JULIAN ASSANGE AMEJITOKEZA HADHARANI KWA MARA YA KWANZA TOKEA
MIEZI MIWILI ILIYOPITA.
ALIZUNGUMZA
KATIKA BARAZA NDOGO KATIKA JENGO LA UBALOZI WA EQUADOR JIJINI LONDON ALIPOKUWA
AMEPATIWA HIFADHI KUEPUKA KUPELEKWA NCHINI SWEDEN KUKABILIANA NA TUHUMA ZA
UBAKAJI.
BWANA
ASSANGE ALIUSHUKURU UBALOZI WA ECUADOR KWA KUMPATIA HADHI YA UKIMBIZI NA
KUIKOSOA VIKALI MAREKANI.
AMESEMA
WASHINGTON NI LAZIMA IAHIDI KUTOMSHITAKI KWA KUFICHUA NYARAKA ZA SIRI NA KUACHA
KILE ALICHOKIITA KUISAKAMA WIKILEAKS.
PIA
AMEZILAUMU NCHI ZA UINGEREZA, SWEDEN NA AUSTRALIA ANAKOTOKA KWA KUSHINDWA
KUMUUNGA MKONO
No comments:
Post a Comment