MAAFISA WA
USALAMA WA LIBYA WAMESEMA MABOMU MAWILI YALIYOKUWA KWENYE GARI YAMELIPUKA
KATIKATI YA MJI MKUU WA TRIPOLI,
MOJA
KARIBU NA OFISI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI NA JINGINE KARIBU NA CHUO CHA
KIJESHI.
TAARIFA
ZINASEMA MILIPUKO HIYO IMEUA WATU WAWILI NA KUACHA WENGINE WANNE KUJERUHIWA
KATIKA CHUO CHA ZAMANI CHA KIJESHI CHA WANAWAKE.
HILI
NI SHAMBULIO KUBWA LA KWANZA KUTOKEA TANGU KUONDOLEWA MADARAKANI KWA ALIYEKUWA
KIONGOZI WA NCHI HIYO MUAMMAR GADDAFI MWAKA JANA.
MKUU
WA USALAMA WA MJI TRIPOLI AMELAANI MASHAMBULIZI HAYO YALIYOLENGWA KWA WATU
WANAOMUUNGA MKONO RAIS WA ZAMANI WA NCHI HIYO MAREHEMU MUMMAR GADDAF.
KATIKA
HOSPTALI YA AL JALAA ILIYOPO TRIPOLI, WESAN ABU ALSOUDE AMBAYE BINAMU YAKE
ALIUAWA AMELAUMU MAMLAKA KWA KUSHINDWA KUCHUCHUKUA HATUA KUZUIA SHAMBULIO HILO.
No comments:
Post a Comment