POLISI
NCHINI AFRIKA KUSINI WAMEWAUA WACHIMBA MIGODI KADHAA NA KUWAJERUHI WENGINE
WENGI KATIKA JUHUDI ZA KUWATAWANYA WAANDAMANAJI WALIOKUWA WAKILALAMIKIA
MISHAHARA DUNI.
MWANDISHI
MMOJA ALIYEKUWEPO NJE YA MGODI WA LONMIN PLATINUM WA MARIKANA ALIAMBIA BBC KUWA
POLISI WALIONEKANA KUSHAMBULIA MFANO WA SIKU ZA UBAGUZI WA RANGI.
WALIOJERUHIWA
WALISAFIRISHWA KWA HELIKOPTA HADI HOSPITALINI.
WAANDAMANAJI
HAO, WACHIMBA MIGODI, WALIKUWA WAKIDAI NYONGEZA YA MSHAHARA WA DOLA 1,500 KWA
MWEZI.
POLISI
WALISEMA MASHAURIANO KATI YA WAWAKILISHI WA WAFANYAKAZI WA ASSOCIATION OF MINE
WORKERS AND CONSTRUCTION (AMCU) YALIKWAMA NA IKALIZIMIKA KUWATIMUA WAFANYAKAZI
HAO KUTOKA MAHALI PALE KWA NGUVU.
POLISI
WALIKUWA WAKIFANYA MAAMUZI WAKATI AMBAPO WACHIMBA MIGODI WALIKUWA WAMESHIKA
MIKONONI SILAHA ZA KITAMADUNI NA BUNDUKI.
RAIS ZUMA
AMENUKULIWA AKISEMA KUWA AMESIKITISHWA SANA NA MAUAJI HAYO YASIYOKUWA NA MAANA.
CHAMA CHA UPINZANI CHA UPINZANI CHA DEMOCRATIC ALLIANCE LIMETOA WITO SERIKALI
KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA KILICHOSABABISHA MAUAJI HAYO.
GHASIA
ZILIANZA MAPEMA JUMA HILI BAADA YA MAKUNDI MAWILI YA KUWAKILISHA WACHIMBA
MIGODI KUPIGANA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU KUMI, KUKIWEMO MAAFISA WAWILAI WA
POLISI.
AFRKA KUSINI
NI TAIFA LINALOZALISHA MADINI AINA YA PLATINUM KWA WINGI ZAIDI DUNIANI.
No comments:
Post a Comment