ECUADOR
IMEKUBALI KUMPA HIFADHI YA KISIASA MWANZILISHI NA MMILIKI WA MTANDAO WA
WIKILEAKS JULIAN ASSANGE.
TANGAZO HILO LIMETOLEWA NA WAZIRI WA
MAMBO YA NJE WA ECUADOR RICARDO PATINO, KWA KILE ALICHOKIELEZA KUWA SERIKALI
YAKE IMEAMUA KUMPAA HIFADHI HIYO KUTOKANA NA WASIWASI WA HAKI ZAKE ZA
KIBINADAMU KUKIUKWA.
PATINO AMEONGEZA KUWA UAMUZI HUO
UMETOLEWA NA SERIKALI BAADA YA MASHAURIANO YA MUDA MREFU NA SERIKALI YA
UINGEREZA NA MAREKANI KUGONGA MWAMBA.
AIDHA, ECUADOR IMEELEZA KUWA UAMUZI
WAKE NI WA KULINDA HAKI ZA WANYONGE KAMA ASSANGE AMBAYE HUENDA AKAULIWA KISIASA
IKIWA ATASAFIRISHWA NCHINI SWEDEN.
UAMUZI HUU WA ECUADOR HUENDA
UKADHOOFISHA UHUSIANO WAKE WA KIDIPLOMASIA NA UINGEREZA .
UINGEREZA IMESEMA KUWA HAITAKUBALI
ASSANGE KUONDOKA NCHINI HUMO LICHA YA ECUADOR KUKUBALI KUMPA HIFADHI YA
KISIASA, KWA KILE INACHOKISEMA KUWA INA HAKI YA KUMKAMATA .
POLISI WAMEKABILIANA NA WAANDAMANAJI
WANAOMUUNGA ASSANGE NJE YA UBALOZI WA ECUADOR JIJINI LONDON NA KUWAKAMATA
WAANDAMAJI WATATU.
ASSANGE RAIA WA AUSTRALIA ALIGONGA
VICHWA VYA HABARI VYA KIMATAIFA BAADA YA KUTOA SIRI AMBAZO ZILIABISHA MATAIFA
MAKUBWA DUNIANI KAMA MAREKANI MWAKA 2010.
JULIAN ASSANGE ANATAKIWA NCHINI
SWEDEN KWA TUHMA ZA UBAKAJI AMBAZO AMEPINGA KUHUSIKA NA KUSEMA NI ZA KISIASA NA
ZINALENGA KUMWANGAMIZA.
TANGU MWEZI WA JUNI ASSANGE AMEKUWA
AKIJIFICHA KATIKA UBALOZI WA ECUADOR JIJINI LONDON UINGEREZA BAADA YA UINGEREZA
KUONESHA NIA YA KUMSAFIRISHA NCHINI SWEDEN KUFUNGULIWA MASHTAKA HAYO YA
UBAKAJI.
SIKU YA JUMATANO ECUADOR ILISHTUMU
UINGEREZA KUWA NA MPANGO WA KUVAMIA UBALOZI WAKE NA KUMKAMATA ASSANGE KWA
NGUVU, TUHMA AMBAZO MTANDAO WA WIKILEAKS UNAKASHIFU .
UINGEREZA IMEKUWA IKISISITIA KUWA INA
HAKI YA KUMSAFIRISHA ASSANGE NCHINI SWEDEN LAKINI ASSANGE MWENYEWE ANAONA KUWA
IKIWA ATAKAMATWA NA UINGEREZA ATASAFIRISHWA MAREKANI NA KUFUNGULIWA MASHTAKA
DHIDI YA UTOAJI WA SIRI ZA SERIKALI HIYO.
No comments:
Post a Comment