Monday, August 13, 2012

BI MAHIZA AMUUNGA MKONO DK MWAKYEMBE


Ben Komba/Pwani-Tanzania/08/13/2012/18:20:40

MKUU WA MKOA WA PWANI BI. MWANTUMU MAHIZA AMEWATAKA WATANZANIA KUUNGA MKONO HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA WAZIRI WA MIUNDOMBINU, BW. HARRISON MWAKYEMBE KATIKA KUHAKIKISHA SUALA LA MIUNDOMBINU NA UCHUKUZI INAKUWA KATIKA KIWANGO KINACHOSTAHILI ILI KURAHISISHA USAFIRISHAJI WA ABIRIA NCHINI NA KATIKA SUALA ZIMA LA KUPUNGUZA AJALI ZA MOTOKAA.

BI. MAHIZA AMEYASEMA HAYO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE LEO, AMBAPO AMESEMA WAKATI WA KUFUKIRIA NJIA NYINGINE INAYOPIGIWA CHAPUO NA WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA UCHUKUZI YA MATUMIZI YA TRENI KWA KUANZIA NA JIJI LA DAR ES SAALAM NA HATA MKOA MWINGINE WA JIRANI WA PWANI NI ZURI NA LA KIMAENDELEO, JAMBO AMBALO ANAAMINI LINAWEZA KUSAIDIA KUPUNGUZA AJALI ZA MARA KWA MARA ZINAZOTOKEA KATIKA BARABARA KUU YA
MOROGORO NA ILE YA KASKAZINI.

MKUU WA MKOA AMEFIKA MBALI NA KUPENDEKEZA UTARATIBU WA KUWAPIMA AKILI MADEREVA KABLA YA KUPATIWA KIBALI CHA KUBEBA ABIRIA KWANI SIKU HADI SIKU AJALI ZIMEKUWA ZIKIONGEZEKA NA NYINGI ZIKIWA ZINASABABISHWA KUTOKANA UZEMBE WA MADEREVA, HARAKA ZISIZO NA MSINGI NA UCHOVU UNAOTOKANA NA MAGARI HAYO KUWA NA DEREVA MMOJA AMBAYE AKIPATA TATIZO LOLOTE BASI SAFARI INAINGIA MASHAKA.

BIBI. MAHIZA AMESISITIZA AJALI SASA KATIKA MKOA WA PWANI ZINATOSHA NA HASA AMEELEZEA KUSIKITISHWA KWAKE NA BAADHI YA WATANZANIA AMBAO WALIKUWA ENEO LA TUKIO LA AJALI ILIYOTOKEA HIVI KARIBUNI KATIKA KIJIJI CHA MAKOLE WILAYANI BAGAMOYO AMBAYO IMESABABISHA VIFO VYA WATU 11 WOTE WAKIWA RAIA WA KENYA, KUANZA KUPIGA PICHA KWANZA KABLA YA KUOKOA MAJERUHI KITENDO AMBACHO AMEKIKEMEA KWA KUKIITA KUWA HAKIPENDEZI NA KIDOGO KINAKARIBIA UNYAMA NA NI WAJIBU WA WATANZANIA INAPOTOKEA AJALI KWENDA ENEO HILO KWA LENGO KUOKOA MAJERUHI NA SIO KUANGALIA KAMA MAONYESHO FULANI.

AMEONGEZA KUWA HAIWEZEKANI NJIA NZIMA KUKAWA NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI ETI KUZUIA AJALI ZISITOKEE HIVYO NI WAJIBU WA MADEREVA KUHAKIKISHA WANAEBNDESHA MAGARI KWA KUZINGATIA KANUNI ZA NENDA KWA USALAMA BARABARANI NA KUHAKIKISHA VIBAO VYA MIONGOZO VVYA KUENDESHA GARI SALAMA WANAVIZINGATIA KATIKA SUALA ZIMA LA KUPUNGUZA AJALI.

No comments:

Post a Comment