Thursday, August 29, 2013

KATIBA CHADEMA



Ben Komba/Pwani-Tanzania/11:22/29-08-2013
Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha wamependekeza kuwa watumishi wote wa serikali wametakiwa kuorodhesha mali zao kabla ya kuanza kutumikia dhamana aliyopewa na nchi ili kutoa fursa kwa yeye kufilisiwa iwapo atatumia madaraka yake vibaya kwa kushiriki vitendo vya ubadhilifu.

Akichangia hoja kuhusiana na rasimu ya Katiba, BW.ISIHAKA MNEMBWE ameomba kuingizwa kwa vifungu vitakavyowezesha wabadhirifu na mafisadi kufilisiwa iwapo watabainika kushiriki vitendo vya kinyume na utaratibu wa utumishi wa umma.

BW.MNEMBWE amebainisha kuwa kuwaacha wabadhirifu wa mali ya umma bila kuchukuliwa hatua madhubuti ambazo zitawagusa moja kwa moja tatizo hilo litabaki kukomaa kutokana na wengine kuamua kufuata mkumbo kutakakosababishwa na kutochukuliwa hatua chanya ambazo zingeweza kuwatia hofu.
Naye mchangiaji mwingine ambaye ni Katibu wa uchumi na Fedha wa CCM kata ya Janga, BW.OTTO KINYONYI amesema katiba mpya ihakikishe kuwa mali na fedha za serikali haziibiwi na wajanja wachache, kwa kutunga sheria kali ambazo zitawabana wabadhirifu

BW.KINYONYI amesisitiza kuwepo na suala uadilifu kwa watumishi wa umma ambao hawatekelezi majukumu na wajibu wao kama watumishi wa umma, na hivyo kusababisha kutokamilika kwa mipango mingi ya kimaendeleo.
Naye Katibu wa CHADEMA Taifa BW. WILBROAD SLAA amewaeleza washiriki wa Baraza hilo la Katiba ambalo limeandaliwa na chama hicho Mkoa wa Pwani, na kufafanua kuwa mwananchi katika nchi yake haki zimeminywa kutokana na kutojua katiba.

BW. SLAA ameongeza kutokujua kwa wananchi suala la Katiba wamekuwa wakiburuzwa katika masuala mbalimbali na kushindwa kuhoji ilihali kila kitu kipo bayana, kutokana na katiba kuweka wazi mambo gani mabaya na mambo gani mazuri kwa ustawi wa Taifa.

No comments:

Post a Comment