Wednesday, August 21, 2013

ABAKA MPWAWE.Ben Komba/Pwani-Tanzania/20-08-2013/10:25

Mkazi mmoja wa mjini Kibaha eneo la Mailimoja ,BW.SEBASTIAN MAGANGA amethibitika kukamatwa kwa kosa la ubakaji wa mwanafunzi mtoto wa mdogo wake.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia Mkaazi huyo akiwa ameongozana na kundi la watu ilihali akiwa mwili mzima umejaa damu akiwa na masikitiko makubwa kutokana na aibu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Pwani, Kamishna msaidizi ULRICH MATEI amebainisha kuwa tukio hilo limetokea eneo la Mailimoja A, ambapo mtuhumiwa huyo ambaye ana mke alikuwa na desturi ya kuamka alfajiri kwenda kwa shangazi yake ambaye wakati huo uwa machinjioni na kumuingilia kimwili binti wa miaka 12 ambaye ni mwanae.

Kutokana na kuwa na mazoea hayo ndipo siku ilipowadia aliponasa katika mtego uliotegwa na shangazi yake mtuhumiwa BIBI. CECILIA MABULA kutokana nay eye kupata taarifa hizo kuhusiana na mwenendo wa kushangaza wa BW.SEBASTIAN MAGANGA mabaye pia alikuwa Katibu mwenezi wa CCM kata ya Mailimoja.

No comments:

Post a Comment