Wednesday, July 17, 2013

SHADRACK Nsajigwa ‘Fusso



SHADRACK Nsajigwa ‘Fusso’ amesema  ameona inatosha kucheza soka la ushindani na hivyo amewaachia vijana waendelee kupambana na ndio sababu ya yeye kugeukia ukocha na kwamba hatakuwa kocha mchezaji.
Beki huyo mwenye heshima kubwa nchini kama alivyo kipa Juma Kaseja aliyetemwa na Simba, amesaini mkataba wa miezi minne wa kuifundisha Lipuli ya Iringa inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
“Ni ngumu kujibu kwa nini nimeamua kuachana na soka, lakini jibu ni rahisi tu, nimepumzika na kuwaachia vijana waendelee, kwani  nimecheza muda mrefu na ni wakati wangu wa kufanya mambo mengine. Kule nakwenda kuwa kocha tu na si kocha mchezaji kwani sitaki tena kucheza mpira kwa sasa,”alisema Nsajigwa.
Nsajigwa amekuwa akishiriki kozi mbalimbali za ukocha za ndani na kuhitimu na amepata  dili la kuifundisha timu hiyo ya mkoani Iringa ambayo itampa mshahara mzurina gharama mbalimbali zikiwemo bima za afya kwake na familia yake.

No comments:

Post a Comment