Saturday, July 20, 2013

MADHARA YA MATUMIZI YA MITANDAO.


Ben Komba/13:30/19/07/2013.

Matumizi ya mtandao yamekuja na changamoto zake ambazo zimesababisha kasi mpya ya mmonyoko wa maadili katika jamii, kutokana na baadhi ya watu kutumia mitandao hiyo kinyume na taratibu zinazongatia ustaarabu na maadili.

Katika tukio moja mwanadada TAUSI SHAABAN mkazi wa mjini Kibaha amejikuta katika wakati mgumu kufuatia rafiki yake ambaye amesoma nae shule ya msingi kumchafua kupitia mtandao wa kijamii PEPERONITY.

Bint. SHAABAN amesema kijana huyo ambaye amefanya hivyo anamkumbuka kwa jina moja la BARAKA ambaye kwa sasa anaishi Mwanza ambaye kwa mara ya mwisho alikutana naye Kituo cha Mabasi ya mkoani Ubungo ambapo kijana huyo alimuomba namba yake ya simu.

Na wakati wakibadilishana namba hizo, Kijana alimuuliza Bint. Shaaban kama ameshazaa na alipojibiwa ndipo alipoaanza kumwambia maneno ya kuudhi na kejeli na kumuahidi kuwa atamkomesha, na ndipo jana ghafla akaanza kupokea simu kutoka kwa wanaume wakware.

Bint. Shaaban ameongeza kuwa mara akaanza kupokea simu kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka kukutana nae kwa lengo la kufanya nao mapenzi kama alivyojitangaza na kuweka namba yake ya simu ya PEPERONITY ili watakaomhitaji wampigie.

Amefafanua kuwa alipowauliza wamepata wapi namba yake ya simu, alijibiwa wameipata katika mtandao huo wa PEPERONITY ambao unajishughulisha na mambo yanayohusiana na ngono kwa kiasi kikubwa, na hivyo kuwa na wakati mgumu kutokana muda wote kupigiwa simu na watu wenye mahitaji ya ngono.

Kutokana na hali hiyo, BINT. TAUSI SHAABAN aliamua kwenda kituo kidogo cha Polisi Mailimoja mjini Kibaha na kutoa maelezo na huku juhudi zikifanyika kumtafua anayehusika na udhalilishaji huo wa kijinsia.

Baadhi ya watu niliongea nao kuhusiana na kadhia hiyo, BW.JOHN GAGARIN ameishauri jamii kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa badala ya kuchafuana na uhalifu kwa faida ya taifa na jamii kwa ujumla.

Naye Kessy GABRIEL mkazi wa Maili moja mjini Kibaha ameitaka TCRA kupambana na vitendo vyote vya matumizi yasiyofaa ya mtandao ili kuepusha usumbufu kwa raia wema unaosababishwa na baadhi ya watu wenye itikadi hasi.

No comments:

Post a Comment