Wednesday, June 19, 2013

BIMA YA AFYA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12:19/17-06-2013

 Mfuko wa Bima ya afya Taifa una mpango wa kuhakikisha unashughulikia kero zote zinazowakabili wanachama wake zinashughulikiwa ili kufikia malengo ambayo imejiwekea wa kutoa huduma sthahili kwa wanachama wa mfuko huo. Mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa Bima ya afya wa Taifa, BW. EMMANUEL HUMBA ameyaongea hayo katika kikao maalum kilichowakutanisha wakuu wa wilaya na watendaji wengine wa mkoa wa Pwani. BW.HUMBA amesema kwa kuanzia watapeleka madaktari bingwa kwa ajili ya wilaya ya Mafia ili kuweza kwenda kutoa huduma kwa wanachama wao wanaosihi na kufanya kazi wilayani humo kutokana na wanachama wao kukabiliwa na tatizo la usafiri wa uhakika. BW. HUMBA amefafanua kuwa kwa wanachama wa mfuko huo wanaosihi Mafia gharama zote za huduma watakazopatiwa zitabebwa na mfuko wa Bima ya afya, wakati wananchi wa kawaida itawalazimu kulipia uchangiaji wa huduma ya afya kama ilivyopangwa na halmashauri au mkoa. Ameongeza madaktari bingwa hao watakuwa katika vituo viwili cha Mafia na katika hospitali maalum ya rufaa ya mkoa, kwa mpango huo madaktari bingwa hao watatolewa Muhimbili, kwa kutambua mahitaji ya wananchi ya kukutana na madaktari bingwa kutokana na kukabiliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya. Naye mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI.MWANTUMU MAHIZA amesema mfuko wa afya umekuwa kimbilio kubwa kwa wananchi ambao kwa muda mrefu walikuwa hawana njia nyingine za kupata matibabu. BIBI.MAHIZA ameongeza kwa sasa wananchi wa mkoa wa Pwani wamehamasika vya kutosha kuhusiana na huduma zinazotolewa na mfuko huo kwani umewaepushia wananchi kuuza mali zao wanapokabiliwa na matatizo ya kiafya ili kujitibu. Aidha amewashukuru watu wa Bima ya afya kuuipatia hospitali ya msaada wa zaidi ya shilingi milioni 300, ikiwa pamoja na kuelekeza kununuliwa kwa chombo cha kupima damu salama ili kuweza kuboresha huduma hiyo katika mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment