Saturday, February 16, 2013

MKURUGENZI SHIRIKA ASHUTUMIWA.





Ben Komba/Pwani-Tanzania/15-Feb-13/18:54:49


Kufuatia kupatikana kwa vipeperushi vinavyosemekana vimechapishwa na wafanyakazi wa shirika la elimu Kibaha zenye kushutumu uongozi wa shirika hilo chini ya Mkurugenzi mtendaji BW. CYPRIAN MPEMBA kwa kupendelea baadhi ya wafanyakazi na kuwaweka wengine pembeni.


Kipeperushi hicho kilichomfikia mwandishi wa habari hizi kikiwa na malalamiko kadhaa yanayomshutumu Mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha kuhusiana na masuala mbalimbali likiwamo kumtaka amuondoe Afisa Tawala wake na kudai kwamba ni mtu anayemshauri juu ya ubaya wa wengine ilihali akificha ya kwake.


Mbali ya lawama hizo kipeperushi hicho kilifika mbali kwa kudai mkurugenzi huyo amekuwa akikataa kutoa fursa kwa wafanyakazi kwenda kujisomea kwa madai ya kuwa shirika halina fedha na wakati huohuo anatoa nafasi kwa mfanyakazi mmoja kwenda kusomea PHD kutokana tu na ukaribu wao.


Akijibu tuhuma hizo Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la elimu Kibaha, DKT. CYPRIAN MPEMBA amesema anachojaribu kufanya yeye ni mabadiliko ya kimuundo ambao utalenga kuimarisha uwezo wa shirika kujitegemea, kitu ambacho kwa sasa hakipo, na kwa kufanya hivyo kwa upande wa hospitali amefanikiwa kuongeza makusanyo ya fedha toka laki nnew kwa siku hadi kufikia milioni 1.6.


DKT. MPEMBA ameongeza mabadiliko hayo yanalenga katika kudhibiti mianya ya uvujaji wawa fedha za shirika la elimu Kibaha kama ilivyokuwa awali, hali ambayo imeliacha shirika katika hali mbaya kimtaji na kunahitajika nguvu ya ziada kulirudisha shirika katika hali yake ya awali.


Kutokana na mabadiliko hayo yenye kulenga kuzuia kutoa ajira kufuata misingi ya ndugu yake ni nani, ikiwa pamoja na kuzuia malipo holela ambapo baadhi ya viongozi walikuwa wanaandika majina wanayoyajua wao na kuamuru walipwe katika mazingira ya kutatanisha na hivyo kulifanya shirika lipoteze fedha nyingi.

No comments:

Post a Comment