Thursday, January 17, 2013

WANANCHI WALIA SHERIA KANDAMIZI HALMASHAURI YA MJI KIBAHA



BEN KOMBA/PWANI-TANZANIA/WEDNESDAY, JANUARY 16, 2013/20:07:27

WANANCHI MJINI KIBAHA WAMELALAMIKIA HATUA YA HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA KUANZISHA SHERIA NDOGONDOGO ZINAZOWAATHIRI KIUCHUMI KUTOKANA NA NYINGI ZA SHERIA HIZO KUWA KANDAMIZI KWA KUWAADHIBU WANANCHI KWA FAINI KUBWA AMBAZO ZIMEKOSA MAKADIRIO SAHIHI.

NIKIONGEA NA MAMA MMOJA MFANYABIASHARA AMBAYE HAKUTAKUTAKA KUTAJA JINA LAKE, AMESEMA MGAMBO HAO WANAOTUMIKA KUWAKAMATA WATU WAMEFIKIA HATUA YA KUZUIA WAFANYABIASHARA KUPANGA BIDHAA ZAO WANAZOZIWEKA MBELE YA MADUKA YAO KWA KISINGIZIO KUWA NI TAKATAKA NA HIVYO KUWAWEKA KATIKA WAKATI MGUMU.

MFANYABIASHARA HUYO AMEELEZEA KUSHANGAZWA KWAKE NA USAFI HUO UNAOFANYWA NA HALMASHAURI YA MJI TOKA HAKUNA VIZIMBA VYA KUTOSHA VYA KUHIFADHIA TAKA NA MATOKEO YAKE TAKATAKA ZINAZOKUSANYWA ZINAENDE KUTUPWA ENEO AMBALO SISTAHILI KUTOKANA NA KUWEPO KARIBU NA MAKAZI YA WATU NA KARIBU MITA 20 KUTOKA OFISI YA KATA AMBALO WAKATI MWINGI KUTOKANA NA MRUNDIKO WA TAKATAKA ENEO HILO HUTOA HARUFU KALI.

MBALI YA HAYO MFANYABIASHARA HUO AMESHANGAZWA NA HAO WATU WANAOSIMAMIA SUALA USAFI WA MAZINGIRA MJINI KIBAHA KWA KUTOITUPIA MACHO OFISI YA KATA YENYEWE AMBAYO IMEKOSA CHOO KWA AJILI MYA WATU WANAOFIKA KUPATA HUDUMA OFISINI HAPO, ENEO AMBALO HATA BWANA AFYA WA KATA ANA OFISI, NA KUITA KINACHOFANYIKA KAMA UKANDAMIZAJI WA WANANCHI.

NAYE KIJANA MJASIRIAMALI WA MAILI MOJA YEYE AMESEMA HALI NI MBAYA MAJUMBANI KUTOKANA NA WATU HAO WANAOAMBATANA NA MGAMBO, KULAZIMISHA WANANCHI KATIKA KILA CHUMBA KULIPIA SHILINGI 700/= ILI TAKA ZAO ZIZOLEWE IKIWA SAWA NA KUWAPIGA MARUFUKU WANANCHI KUTAFUATA NJIA ZAO WENYEWE ZA KUHIFADHI TAKA HIZO BILA KULETA ATHARI.

KIJANA HUYO AMEMTAJA KADA MMOJA WA CHAMA CHA MAPINDUZI NDIYE ANAYEONGOZA HARAKATI HIZO, NA KUITA KITENDO HICHO NI CHA KIBEPARI NA KINADHULUMU HAKI ZA WANANCHI KWA KUANISHA SHERIA NDOGONDOGO MBALIMBALI AMBAZO ZINAKUWA NA ATHARI KWA MWANANCHI KIUCHUMI, AMEOMBA WIZARA YA SERIKALI ZA MITAA KUANGALIA KODI NDOGONDOGO ZINAZOTUNGWA NA HALMASHAURI KWANI NYINGI NI KANDAMIZI.

NAYE BWANA AFYA WA KATA YA MAILI MOJA, BW. ALLY BAKAR SHAH AMEENDELEA KUSISITIOZA SUALA LA USAFI NI SUALA AMBALO LIPO SIKU NYINGI NA KILA MMOJA ANALITAMBUA NA ELIMU IMEKUWA INATOLEWA KWA WANANCHI ILI WAWEZE KUELEWA LENGO HASA LA UTARATIBU HUO MPYA AMBAO AMEWAHAKIKISHIA WANANCHI UTAENDELEA KUWEPO TOKA HIZO NI SHERIA NDOGO ZA HALMASHAURI, AIDHABW. SHAH AMEKANUSHA KUTOKUWEPO KWA CHOO KATIKA OFISI YA KATA YA MAILI MOJA.

No comments:

Post a Comment