Saturday, January 26, 2013

WAKALIMANI WA LUGHA ZA ALAMA WAHITAJIKA KUWASAIDI VIZIWI.


BEN KOMBA/PWANI-TANZANIA/26-JAN-13/18:11:47

CHAMA KINACHOFANYA UTAFITI JUU YA WATU WASIOSIKIA NCHINI, (TADERE} KIMEFANYA WARSHA MAALUM KWA WAZAZI NA WALIMU WENYE WATOTO WALEMAVU NA MAOFISA WATENDAJI WA VIJIJI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA KIJAMII KWA WATU WASIOSIKIA AMBAO WAMEKUWA WAKIPITWA NA MAMBO MBALIMBALI KUTOKANA NA HALI YAO.

MKURUGENZI WA TADERE, BW. NIDROSY MLAWA AMESEMA WATU WENYE MATATIZO YA KUSIKIA WAMEKUWA WAKIACHWA NYUMA KATIKA MASUALA MBALIMBALI KUTOKANA NA UKOSEFU WA WAKALIMANI WA KUTOSHA KUWATAFSIRIA MATAMKO MBALIMBALI YANAYOTOLEWA NA SERIKALI NA KUSABABISHA USHIRIKI WAO KUWA MDOGO KAMA KATIKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA UNAOOENDELEA.

BW. MLAWA AMEBAINISHA JAMII LAZIMA IKUMBUKE KUWA WALEMAVU WA KUSIKIA NAO WANA WAJIBU WA KUPATA HUDUMA ZA KIROHO NA HIVYO AMESHAURI WAKATI SASA UMEFIKA KWA MADHEHEBU YA DINI MBALIMBALI KUWEKA MAZINGIRA AMBAYO YATAMUWEZESHA MTU ASIYESIKIA KUPATA HUDUMA HIYO YA KIROHO.

NAYE KAMISHNA MSTAAFU WA USTAWI WA JAMII TANZANIA, BW. NNYAPULE MADAI AMBAYE ALIKUWA MWEZESHAJI KATIKA WARSHA HIYO AMEWAAMBIA WASHIRIKI KUWA KIPINDI CHA AZIMIO LA ARUSHA SUALA LA KUSHUGHULIKA NA WALEMAVU LILIKUWA NI LA SERIKALI, NA LILIWAZUNGUMZIA KAMA NI KUNDI AMBALO LINAHITAJI KULELEWA SAWA NA WATOTO NA WAZEE NA WENGINE WOTE AMBAO MAUMBILE YAO YANAWAFANYA WASHINDWE KUFANYA SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI.

BW. MADAI AMEFAFANUA KWA SASA TANZANIA INA WALEMAVU TAKRIBAN MILIONI 4 IKIWAZINGATIA SENSA YA MWAKA 2012, LAKINI CHANGAMOTO KUBW WANAZOKABILIANA NAZO NI WALIMU WENGI KUTOKUWA NA UTAALAMU WA KUGUNDUA WATOTO WENYE MATATIZO YA KUSIKIA NA BAADHI YA VYUO VYA UFUNDI KUKOSA MAZINGIRA RAFIKI KWA WATU WENYE ULEMAVU WA AINA YOYOTE ILE.

BW. MADAI AMEONGEZA KUYWA KUKOSEKANA KWA NYENZO ZA KUJIMUDU KWA WATU WENYE ULEMAVU KAMA VIKUZA SAUTI KWA WATU WASIOSIKIA, FIMBO NYEUPE KWAN WALEMAVU WA KUONA, NA MAFUTA YA KUJIPAKA, MIWANI NA KOFIA KWA AJILI YA WATU WENYE WALEMAVU WA NGOZI NA VITI VYA MAGURUDUMU KWA WALEMAVU WA VIUNGO, AIDHA AMEZITAKA TAASISI AMBAZO ZINATOA MISAADA KUHAKIKISHA ZINATOA VIFAA VYENYE UBORA UNAOTAKIWA BADALA YA KUWAPATIA VIFAA AMBAVYO VINGI HAVIDUMU HATA MIEZI MITATU VINAHARIBIKA HASA UPANDE VITI VYA MAGURUDUMU.

No comments:

Post a Comment