
WANAJESHI WA NIGERIA WAMESEMA WAMEMTIA NGUVUNI KIONGOZI MMOJA
WA KUNDI LA WAPIGANAJI WA BOKO HARAM KASKAZINI MWA NCHI HIYO.
TAARIFA ZINADOKEZA KUWA KIONGOZI HUYO MOHAMMED ZANGINA
ALITIWA NGUVUNI KATIKA MJI WA MAIDUGURI.
WANAJESHI HAO WANADAI ZANGINA ALIHUSIKA KUPANGA MASHAMBULIZI
YA KUJITOLEA MUHANGA KATIKA MIJI KADHAA.
JESHI LA NIGERIA LILIKUWA LIMETANGAZA ZAWADI YA DOLA LAKI
MOJA NA SITINI KWA YEYOTE ATAKAYEMKAMATA KIONGOZI HUYO.
KIKOSI MAALUM CHA JESHI KILISEMA KILIMKAMATA ZANGINA MAPEMA
JUMAPILI KATIKA MTAA MMOJA WA KIFAHARI MJINI MAIDUGURI AMBAKO NDIO NGOME YA
HARAKATI ZA BOKO HARAMA.
HATA HIVYO DURU ZINASEMA KUWA JESHI LA NIGERIA WAKATI
MWINGINE HUONGEZA CHUMVI MADAI YAKE KUHUSIANA NA KUNDI HILO AMBALO LIMEHUSIKA
NA MASHAMBULIZI KADHAA KASKAZINI MWA NCHI.
TAARIFA YA JESHI ILISEMA KUWA ALIKUWA MJINI MAIDUGURI KUPANGA
MASHAMBULIZI DHIDI YA RAIA NA MAAFISA WA USALAMA
LIKITAJA MIJI KADHAA NCHINI HUMO, JESHI LILISEMA KUWA ZANGINA
NDIYE AMEKUWA AKIONGOZA MASHAMBULIZI KATIKA MIJI HIYO IKIWEMO ABUJA, KADUNA,
KANO, JOS NA POTISKUM."
JESHI LIMEKUWA LIKIDAI KUWAKAMATA VIGOGO WA KUNDI HILO KATIKA
MIEZI YA HIVI KARIBUNI INGAWA HAKUNA UHAKIKA IKIWA BOKO HARAM IMEATHIRIKA KWA
VYOVYOTE.
No comments:
Post a Comment