Monday, January 14, 2013

AUWAWA KWA UVAMIZI


BEN KOMBA/PWANI-TANZANIA/14/01/2013/16:13:17

MTU MMOJA AMEUWAWA NA WATU WENYE HASIRA KALI KUFUATIA KUVAMIA NYUMBA YA BI. MWAJUMA SHAABAN KATIKA ENEO LA KWA MATHIAS MJINI KIBAHA LEO MAJIRA YA ALFAJIRI BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NDANI YA NYUMBA.

MWANDISHI WA HABARI HIZI AKIONGEA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA PWANI, KAMISHNA MSAIDIZI ULRICH MATEI AMESEMA TUKIO HILO LIMETOKEA ALFAJIRI YA LEO AMBAPO JAMBAZI HUYO AKIWA NA WENZIE WALIVAMIA NYUMBA YA DADA HIYO.

KAMANDA MATEI AMEBAINISHA KUWA MTU HUYO AMBAYE HAJULIKANI JINA LAKE WALA MAHALI ANAPOISHI ANAKADIRIWA KUWA NA UMRI YA MIAKA 20 MPAKA 25 ALIUWA KWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA MWIZI HUYO NA WENZIE WATATU KUVAMIA NYUMBA YA BI. MWAJABU SHAABAN AMBAYE NI MFANYABIASHARA.

AMBAPO WALIFANIKIWA KUINGIA NDANI KWA MFANYABIASHARA HIYO ANAYEISHI MAENEO YA UMWERANI KWA MATHIAS KWA KUVUNJA MLANGO KWA KUTUMIA JIWE LA FATUMA, WALIIBA DVD PLAYER MOJA YENYE THAMANI YA SHILINGI YA 65,000, FEDHA TASLIMU SH.400,000 NA SIMU MBILI AINA YA TECHNO YENYE THAMANI YA SHILINGI 100,000.

KAMANDA MATEI AMEONGEZA KUWA KATIKA ENEO LA TUKIO KULIPATIKANA WAYA WA KUFYATULIA BARUTI AMBAO WEZI HAO WALITUMIA KUWATISHIA WENYE NYUMBA.
KUKAMATWA KULIKUJA BAADA YA BI. MWAJABU SHAABAN KUTOA TAARIFA KWA NJIA YA SIMU YA MKONONI KWA BAADHI YA MAJIRANI ZAKE KWA KUTUMIA SIMU YAKE YA MKONONI WAKATI MAJAMBAZI HAYO YAKIWA KATIKA CHUMBA CHA WATOTO NA KUFANIKIWA KUKAMATWA KWA JAMBAZI HILO AMBALO BAADAYE LILIUWAWA.

No comments:

Post a Comment