Monday, December 24, 2012

MAKABURI YA KALE YAVUNJWA TIMBUKTU

TAARIFA KUTOKA KASKAZINI MWA MALI ZINAELEZA KUWA WAPIGANAJI WA KIISLAMU WAMEVUNJA MAKABURI KADHA YA KALE KATIKA MJI WA TIMBUKTU.
KIONGOZI MMOJA WA WAPIGANAJI HAO AMELIAMBIA SHIRIKA LA HABARI LA UFARANSA KWAMBA MAKABURI YOTE MJINI TIMBUKTU YATAVUNJWA, KWA SABABU YANAKWENDA KINYUME NA UISLAMU.

 
KATI YA MWAKA HUU MAKABURI KADHA YALIVUNJWA KATIKA MJI HUO AMBAO NI ENEO LA KUHIFADHIWA KUFUATANA NA UMOJA WA MATAIFA.
MAKUNDI YA WAPIGANAJI WA KIISLAMU NA MENGINEYO YALITEKA ENEO LA KASKAZINI LA MALI BAADA YA SERIKALI YA TAIFA KUPINDULIWA AWALI MWAKA HUU.
SIKU YA ALKHAMISI UMOJA WA MATAIFA ULIPITISHA AZIMIO KUKUBALI KIKOSI CHA NCHI ZA AFRIKA KUTUMWA MALI.

No comments:

Post a Comment