Friday, September 28, 2012

ZITTO KABWE YUPO SERIOUS NA SUALA LA URAIS 2015






“NIMEFANYA KAZI KUBWA KATIKA KAZI YANGU YA UBUNGE, NIMELETA MABADILIKO MENGI KUANZIA BUNGENI  MPAKA JIMBONI. NADHANI INATOSHA NA HATA NIKIONGEZEWA MIAKA MINGINE SITAWEZA KUFANYA YALE YALIYONISHINDA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA KUMI.
 
“KAMA MUNGU ATANIWEKA MPAKA MWAKA 2015, SITAGOMBEA UBUNGE TENA KWA SABABU KAZI NILIYOFANYA INATOSHA. NATANGAZA RASMI KUWA NITAGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHANGU CHA CHADEMA, BILA KUSABABISHA MSUGUANO WOWOTE NA SITAKI KUINGIA KATIKA HISTORIA YA KURUDISHA NYUMA HARAKATI ZA UPINZANI KUSHIKA DOLA,” ALISEMA ZITTO.
 
HATA HIVYO ZITTO ALIPOULIZWA BAADAYE NA MWANANCHI KUWA MWAKA 2015 ATAKUWA NA MIAKA 39, HIVYO KUKOSA SIFA YA KUGOMBEA URAIS KWA MUJIBU WA KATIBA ALIJIBU; “NADHANI NINA UWEZO WA KUWA RAIS, SIDHANI KAMA KATIBA INAWEZA KUMZUIA MTU MWENYE UWEZO ASIGOMBEE NA NDIO MAANA NINAAMINI KUWA KIPENGELE CHA KUWA NA MIAKA 40 KITABADILISHWA KATIKA KATIBA MPYA.”

“NCHI ZA KIDEMOKRASIA LAZIMA VYAMA VIBADILISHANE UTAWALA WA KUONGOZA NCHI  KAMA ILIVYO KATIKA NCHI ZA GHANA NA ZAMBIA. TANZANIA INATAKIWA KUIGA MFANO WA NCHI HIZO,” ALISEMA ZITTO

No comments:

Post a Comment