Friday, September 28, 2012

RUNGU LA MWANGUKIA TERRYJOHN TERRY AMEADHIBIWA NA CHAMA CHA KANDANDA CHA ENGLAND, FA, ASICHEZE MECHI NNE, NA VILE VILE ALIPE FAINI YA PAUNI 220,000, KUTOKANA NA MATAMSHI YA UBAGUZI WA RANGI DHIDI YA MCHEZAJI WA QPR, ANTON FERDINAND. 

CHAMA CHA FA KILITHIBITISHA TERRY ALIFANYA MAKOSA HAYO, BAADA YA KUSIKILIZA KESI DHIDI YAKE KWA KIPINDI CHA SIKU NNE. 

MSEMAJI WA JOHN TERRY ALISEMA MCHEZAJI HUYO "ALISIKITISHWA" NA HATUA YA FA, KWA KUAMUA TOFAUTI, KINYUME NA MAHAKAMA, AMBAYO AWALI ILISEMA HANA MAKOSA.

MWEZI JULAI, MAHAKAMA YA WESTMINSTER MJINI LONDON ILIPITISHA UAMUZI KWAMBA MCHEZAJI HUYO, MWENYE UMRI WA MIAKA 31, HAKUFANYA KOSA HILO, LA KUTUMIA MATAMSHI YA UBAGUZI WA RANGI DHIDI YA FERDINAND.

No comments:

Post a Comment