Saturday, September 29, 2012

YALIYO WAKUTA BAADHI YA WAGOMBEA WA NAFASI MABALIMBALI CCM


ATIKA BUNGE LA 10 LILILOKETI APRILI MWAKA HUU, BAADHI YA WABUNGE WA CCM AKIWAMO FILIKUNJOMBE, MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI, NIMROD MKONO NA MBUNGE WA MWIBARA, KANGI LUGOLA, WALIUNGA MKONO HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA PINDA ILIYOKUWA IMEANZISHWA BUNGENI NA 

MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI, ZITTO KABWE WA CHADEMA.



SIKU MOJA BAADA YA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC), KUTANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA, BAADHI YA VIGOGO WALIOACHWA KWENYE UTEUZI HUO WAMEELEZA YA MOYONI, HUKU MBUNGE WA LUDEWA, DEO FILIKUNJOMBE AKISEMA ANAAMINI AMETOSWA KWA SABABU ALITIA SAINI YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA.

DEO FILIKUNJOMBE

 

"NIMESAINI KITABU KILE KWA NIA NJEMA, NIKIWA NA AKILI TIMAMU NA SIJUTII UAMUZI WANGU HUO, ILA SIWEZI KUWASEMEA KIGWANGALLA (KHAMIS MBUNGE WA NZEGA) NA BASHE (HUSSEIN). LAKINI SISI WATATU (YEYE, LUGOLA, MKONO) TUMEENGULIWA KWA SABABU HIYO (YA KUTOKUWA NA IMANI NA PINDA). ALIENDELEA: "NASHANGAA LEO NAONEKANA ADUI WA CHAMA WAKATI NILIKUWA NAKINUSURU NA KUSEMA KWELI ADUI WA CCM NI WABUNGE WA CHAMA HICHO AMBAO HAWAKUSAINI KITABU HICHO CHA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU, " ALISEMA FILIKUNJOMBE."

NIMROD MKONO


 ALISEMA HUU NI UTARATIBU WA CHAMA CHAO CHA CCM AMBAO UMEWAPA BAADHI YA WATU HAKI YA KUWAFUKUZA WENGINE BILA KUWAPA FURSA YA KUJITETEA.

 "KAMA ILIVYOTOKEA KWANGU WAMEKAA NA KUONA MKONO HAFAI, FUKUZA BASI WAKAFANYA HIVYO NA HIYO HAIJALISHI KAMA NILISAINI KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU AU LA.  SUALA LA MSINGI NI KUWA MKONO AMEFUKUZWA NA ATARUDI KAMA ILIVYOKUWA KWA MWANA MPOTEVU." ALISEMA BILA KUFAFANUA.

 DK KIGWANGALLA.



“NITAENDELEA KUHESHIMU VIKAO VYA CHAMA CHANGU NA KUWA MWANACHAMA HAI INGAWA SIJAJUA WAMETUMIA VIGEZO GANI KUTEUA MAJINA HAYO,” 

BASHE


BASHE ALISEMA KILICHOTOKEA NI UAMUZI WA CHAMA NA VIKAO HALALI VILIVYOKAA NA KUCHUKUA UAMUAZI HUO.

“SIJUI KWA NINI JINA LANGU HALIKUPITISHWA, LAKINI NITAENDELA KUWA MWANACHAMA NA KUWATUMIKIA WANANCHI WENZANGU WA NZEGA,” ALISEMA BASHE.

No comments:

Post a Comment