Chama cha
wananchi CUF kinajiandaa kwenda mahakamani kupinga ushindi wa mgombea wa CCM
Hussein Ibrahim Makungu katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu uliofanyika
Jumapili iliyopita.
Akizungumza
na Zenji FM radio, mkuregenzi wa mawasiliano na haki za binadamu wa CUF Salim
Bimani amesema wanasheria wa chama hicho wanaandaa taratibu za kisheria ili
kufungua kesi hiyo.
Amesema wana
ushahidi wa kutosha wa kukiukwa taratibu za uchaguzi ikiwemo upandikizaji wa
wapiga kura.
Bimani
amesema taratibu za kisheria za kufungua madai hayo zinatarajiwa kukamilika
ndani ya siku 14 tokea kutangazwa mshindi huyo.
Chama cha
wananchi CUF kimepinga matokeo ya uchaguzi yaliompa ushindi mgombea wa CCM
Makungu kwa kupata asilimi 50.7 ya kura dhidi ya mgombea wa CUF Issa Khamis
Issa aliepata asilimia 48.2 ya kura.
Wakati huo
huo mbunge wa jimbo la Mtoni Faki Haji Makame amekanusha taarifa za kukamatwa
na jeshi la polisi na kufikishwa mahakamani akidaiwa kupigana hadharani siku ya
uchaguzi huo.
Akizungumza
na wandishi wa habari huko afisi ya wilaya CUF Vuga amesema taarifa hizo
alizonukuliwa kamishna wa polisi Zanzibar zina lengo la kupotosha ushahidi
dhidi ya kadhia ya kupigwa iliyomkuta siku hiyo.
Makame
amesema siku ya tukio hilo alipigwa na vijana watatu kati yao wawili
walikamatwa na jeshi la polisi kituo cha Bububu, lakina anashangazwa bado
hawajafunguliwa mashtaka
No comments:
Post a Comment