Wednesday, September 12, 2012

MKUU WA WILAYA AMKWIDA DIWANI KWENYE KARAMU


MKUU WA WILAYA YA KAHAMABENSON MPESYA


JUZI ALIMKWIDA NA KUMUONDOA KATIKA MSTARI WA VIONGOZI KWENDA KUPATA CHAKULA, DIWANI WA KATA YA NYIHOGO (CHADEMA), AMOS SIPEMBA.

CHAKULA HICHO KILIKUWA MAALUM KWA MSAFARA WA WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA.


MKUU HUYO WA WILAYA AMBAYE ALIONEKANA KUWA MAKINI ZAIDI NA UGENI HUO
BAADA YA KUMALIZA KUTANGAZA WAGENI WA KIMKOA, ALIWACHAGUA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA

KADHALIKA DIWANI WA KAHAMA MJINI ILI WAUNGANE NA MSAFARA HUO KATIKA UPATA CHAKULA.

IWANI SIPEMBA AKIWA NA MWENZAKE WA KATA YA MWENDAKULIMA (TLP), NTABO MAJABI NAO WALIJIPACHIKA KWENYE MSTARI WAKIWA NYUMA YA DIWANI WA KATA YA KAHAMA MJINI, ABASI OMARI, AMBAYE MPESYA ALIMTAKA AJUMUIKE NA UGENI KUTOKA MKOANI.

LAKINI ALIPOONA SIPEMBA YUKO MSTARINI, MKUU HUYO WA WILAYA ALIKWENDA NA KUMTAKA ASIINGIE KWENYE MSTARI LAKINI DIWANI HUYO ALIKAIDI AMRI.

KITENDO HICHO KILIMFANYA MPESYA AMPIGE JEKI KWA NYUMA KWA KUTUMIA MKANDA WA SURUALI ALIYOKUWA AMEVAA (DIWANI) NA KUMNYANYUA MITHILI YA MHALIFU.


No comments:

Post a Comment