Thursday, September 27, 2012

MIAKA KADHAA IJAYO


MIAKA MICHACHE IJAYO, IBADA ZITAKUWA KAMA IFUATAVYO.

MCHUNGAJI: BWANA ASIFIWEEEEE!

WAUMINI: AMEEEEEEEEENI!

MCHUNGAJI: TAFADHALINI WASHARIKA SASA TUCHUKUE IPAD, TABLET PC, SIMU NA KINDLE ZETU ILI TUFUNGUE 1 WAKORINTHO 13:13. PIA WASHENI BLUETOOTH ZENU ILI MUWEZE KUPOKEA MAHUBIRI. MNAOTUMIA FACEBOOK, TWITTER, BBM NA WHATSAPP MNAWEZA KUENDELEA KUPOKEA MAHUBIRI HAYA. TAFADHALINI WASHARIKA MNAWEZA KUTUMIA WI-FI YA KANISA KWA UHURU KABISA KWA KUTUMIA NYWILA YA IMANI613. HALELUUUUUUUYAH!

WAUMINI: HALELUUUUYAAAAAAAAH!

MCHUNGAJI: WAPENDWA WASHARIKA SASA NI WAKATI WA SADAKA KWA HIYO KADRI YA ITAKAVYOKUPENDEZA KUMTOLEA MUNGU UNAWEZA KUTUMIA CREDIT AMA DEBIT CARD, PIA UNAWEZA KUTOA SADAKA KWA NJIA YA MPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY AMA ZPESA KUPITIA NAMBA ZINAZOONEKANA KWENYE SKRINI.

WAKATI WA MATANGAZO
KATIBU WA USHARIKA: WAPENDWA WASHARIKA WIKI HII KUTAKUWA NA MIKUTANO YA KIROHO KUPIGIA GROUP LETU LA FACEBOOK. MADA KUU ITAKUWA UPONYAJI WA KIROHO KWENYE NDOA. WASHARIKA WOTE MNAKARIBISHWA KUSHIRIKI.

SIKU YA ALHAMISI KUTAKUWA NA MAFUNDISHO YA BIBLIA MOJA KWA MOJA KUPITIA SKYPE KUANZIA SAA MOJA JIONI. TAFADHALI MSIKOSE KUSHIRIKI. PIA MNAWEZA KUENDELEA KUFUATILIA IBADA HII PAMOJA NA MAFUNDISHO YOTE KUTOKA KWA MCHUNGAJI KUPITIA AKAUNTI YAKE YA TWITTER.

No comments:

Post a Comment