Friday, September 21, 2012

MAHAKAMA YAFUTA HATI YA KUKAMATWA MBOWE 

MAHAKAMA YA WILAYA YA HAI IMEFUTA HATI YA KUKAMATWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA), FREEMAN MBOWE, ILIYOTOLEWA BAADA YA KUSHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI KUJIBU TUHUMA ZINAZOMKABILI.

MAHAKAMA HIYO ILIMFUTIA MBOWE NA MDHAMINI WAKE, AWADH MUSSA, BAADA YA KUPOKEA MAELEZO NA VIELEZO.

AKITOA VIELEZO NA MAELEZO MAHAKAMANI HAPO JANA YALIYOSABABISHA KUSHINDWA KUHUDHURIA MAHAKAMANI HAPO, MDHAMINI HUYO ALIMUELEZA HAKIMU MFAWIDHI WA WILAYA HIYO, DENNIS MPELEMBWA, KWAMBA SIKU YA KESI ALIKUWA MGONJWA NA ALILAZWA HOSPITALI NA KUSHINDWA KUFIKA.

ALISEMA MTUHUMIWA ALISHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI HAPO KUTOKANA KUWA NJE YA NCHI KWA AJILI YA SHUGHULI ZA KISERIKALI AKIWA KAMA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI.

KUTOKANA NA SABABU HIZO, HAKIMU MPELEMBWA HAKUWA NA PINGAMIZI NA KUFUTA HATI YA KUMKAMATA NA KUTOA AMRI YA MTUHUMIWA HUYO KUFIKA MAHAKAMANI TAREHE ITAKAYOPANGWA KWA AJILI YA KUENDELEA NA HATUA YA USIKILIZAJI.

AWALI ILIDAIWA KUWA MBOWE ANAKABILIWA NA MASHITAKA YA KUFANYA VURUGU NA KUMJERUHI MSIMAMIZI WA UCHAGUZI, NASRI OTHMANI, SIKU YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2010 KATIKA KITUO CHA LAMBO.

INADAIWA MSHITAKIWA HUYO ALIMSHAMBULIA MSIMAMIZI HUYO NA KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI MWILINI.

MBOWE AMESHITAKIWA KUTOKANA NA KUVUNJA KIFUNGU CHA SHERIA YA MAKOSA YA JINAI KIFUNGU CHA 240 SURA YA 16 YA SHERIA ZA TANZANIA, KUTOKANA NA KUFANYA SHAMBULIO HILO KATIKA KIJIJI HICHO SAA 11 JIONI.

PAMOJA NA KUFUTA HATI YA KUMKAMATA MBOWE, KESI HIYO ILIPANGWA KUSIKILIZWA TENA OKTOBA 9, MWAKA HUU.

No comments:

Post a Comment