Sunday, September 2, 2012

KIFO CHA MWANAHABARI KATIKA VURUGU ZA KISIASADAUD MWANGOSI KULIA ENZI ZA UHAI DAKIKA 20 KABLA YA KUUWAWA KWAKE

MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN MKOA WA IRINGA NA MWENYEKITI WA CHAMA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA IRINGA DAUD MWANGOSI AMEUWAWA KATIKA VURUGU ZA POLISI NA WAFUASI WA CHADEMA KATIKA KIJIJI CHA NYOLOLO WILAYA YA MUFINDI MKOANI IRINGA LEO.

MWANAHABARI HUYO DAUD MWANGOSI ALIUWAWA MAJIRA YA SAA 10 JIONI KATIKA OFISI ZA CHADEMA NYOLOLO HUKU ASKARI MMOJA AKIJERUHIWA VIBAYA KWA RISASI.

KABLA YA KUUWAWA KWA MWANAHABARI HUYO MABOMU YALIWEZA KUPIGWA ENEO HILO KUWATAWANYA WAFUASI HAO WA CHADEMA AMBAO WALIKUWA WAKIGOMA KUTAWANYIKA ENEO HILO NA KUAMUA KUKAA CHINI KUWA HAWAPO TAYARI KUONDOKA KATIKA OFISI YAO.

CHANZO CHA MWANAHABARI MWANGOSI KUUWAWA KILITOKANA NA KUKAMATWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA NIPASHE MKOA WA IRINGA, GODFREY MUSHI NA HIVYO MWANAHABARI HUYO KUTAKA KUHOJI POLISI SABABU YA KUKAMATWA KWA MWANAHABARI HUYO, NDIPO ASKARI HAO WALIPOANZA KUMSHAMBULIA KWA KICHAPO NA BAADAE MLIO KAMA WA BOMU ULISIKIKA ENEO HILO NA MWANDISHI HUYO NA ASKARI MMOJA WALIAGUKA CHINI.

NDANI YA DAKIKA TANO ILISIKIKA SAUTI KUTOKA KWA ASKARI HUYO KUWA 'AFANDE NIMEKUFA' NDIPO WALIPOMCHUKUA NA KUMPELEKA HOSPITALI YA WILAYA YA MUFINDI HUKU MWILI WA MWANAHABARI HUYO UKIPELEKWA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI.

KATIKA VURUGU HIZO ZILIZODUMU KWA TAKRIBANI DAKIKA 30 KWA ASKARI NA WAFUASI WA CHADEMA KURUSHIANA MAWE KWA MABOMU ZAIDI YA MAGARI MATANO YA CHADEMA NA YA WANANCHI YAMEHARIBIWA HUKU WATU KADHAA WAMEJERUHIWA NA MWANAHABARI MMOJA GODFREY MUSHI AKIJERUHIWA VIBAYA

No comments:

Post a Comment