WANACHAMA NA WAFUASI WA CHADEMA WAKIWA NJE YA MAHAKAMA KUU KANDA YA KASKAZINI KUSIKILIZA KINACHOENDELEA.

Godbless Lema anaepinga kuenguliwa ubunge wake na Mahakama Kuu kanda ya Arusha akijiandaa kuingia katika usafiri wake kuondoka katika viwanja vya Mahakama Kuu Arusha asubuhi ya leo

Umati wa watu nje ya uzio wa Mahakama Kuu Arusha kumlaki Mh Lema akitoka Mahakamani

Msafara unaondoka, haikuwa rahisi kuwazuia watu hawa kusindikiza gari ya Mh Lema

Waanausalama wapo kazini, nyuma ya msafara

Msafara umeingia Old Moshi Road kuelekea Ngarenaro. Wananchi hawa walijawa na furaha na kujikuta wakiimba nyimbo za mashujaa kwa sauti huku wakipeperusha matawi ya miti na majani

Baadhi ya wananchi walioamaua kutangulia Ofisini

Msafara unakatiza mitaa ya Jiji kuingia mjini kabisa

Wananchi hawa walikuwa wamejipanga kando ya barabara na kujikuta wameshindwa kujizuia hisia zao

Wanawasili eneo zilipo ofisi za Chadema, Ngarenaro

Gari iliyombeba Lema ikiwa imezingirwa ofisini hapo mara baada ya kuwasili

Wakiitikia “Peoples Power” iliyoimbishwa na Lema ambae haonekani pichani

Kamanda wa Chadema mjini Arusha maarufu kama Omari Matelephone akiwa amejitupia pamba zake zenye nakshi ya rangi zinazopatikana katika bendera ya chama hicho.
No comments:
Post a Comment