Thursday, September 13, 2012

JOPO LA KESI YA LEMA WA ARUSHA MJINI


JAJI MKUU WA TANZANIA, MOHAMED CHANDE OTHMAN, ATAUNGANA NA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA, NATALIA KIMARO NA SALUM MASSATI, KUSIKILIZA RUFAA YA KUPINGA KUVULIWA UBUNGE YA ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO LA ARUSHA MJINI, GODBLESS LEMA (CHADEMA), AKICHUKUA NAFASI YA JAJI MBAROUK SALIM MBAROUK.

KWA MUJIBU WA RATIBA YA VIKAO VYA MAHAKAMA HIYO ILIYOSAINIWA NA NAIBU MSAJILI WA MAHAKAMA YA RUFAA, MALEWO, AMBAYO IMEBANDIKWA KWENYE UBAO WA MATANGAZO INAONYESHA KUWA MABADILIKO HAYO YATAANZA SEPTEMBA 20, MPAKA MWISHO WA VIKAO HIVYO OKTOBA MOSI MWAKA HUU.
KWA UPANDE WAKE, WAKILI WA LEMA, METHOD KIMOMOGORO, ALISEMA ATASHIRIKIANA NA WAKILI MWENZAKE TUNDU LISSU KATIKA SHAURI HILO LITAKALOSIKILIZWA KWA SIKU MOJA NA KUPANGIWA TAREHE YA KUSOMWA HUKUMU, ALIONGEZA KUWA TAYARI ALISHAITAARIFU MAHAKAMA JUU YA SUALA HILO TOKEA AGOSTI 28, MWAKA HUU.

UAMUZI HUO WA LISSU KUMWAKILISHA LEMA KWENYE SHAURI HILO UTAMKUTANISHA MAHAKAMANI HAPO NA KAKA YAKE, WAKILI, ALUTE MUGHWAI ANAYEWAWAKILISHA WANACHAMA WATATU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), MUSSA MKANGA, AGNESS MOLLEL, NA HAPPY KIVUYO, WALIOFUNGUA SHAURI LILILOPELEKEA KUTENGULIWA KWA UBUNGE WA LEMA WAKIDAI KUWA WAKATI WA KAMPENI MBUNGE HUYO ALIMDHALILISHA MGOMBEA WA CCM, DK. BATILDA BURIAN, KWA KUTUMIA LUGHA YA MATUSI.

AWALI LEMA KUPITIA WAKILI WAKE, KIMOMOGORO, ALIWASILISHA KWENYE MAHAKAMA HIYO HOJA 18 ZA MADAI AKIPINGA KUTENGULIWA KWA UBUNGE WAKE NA MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA APRILI 5, MWAKA HUU.

KWENYE BAADHI YA MADAI HAYO, LEMA ALIIOMBA MAHAKAMA YA RUFAA KUTENGUA UAMUZI WA MAHAKAMA KUU, ULIOTENGUA UBUNGE WAKE, HUKU AKIITAKA IMTANGAZE KUWA MBUNGE HALALI WA JIMBO LA ARUSHA MJINI.
AIDHA, ALIITAKA MAHAKAMA HIYO YA JUU, IWAAMURU WALALAMIKIWA KATIKA SHAURI HILO WALIPE GHARAMA ZA RUFAA HIYO PAMOJA NA ZILE ZA KESI ILIYOMALIZIKA KWENYE MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA.

KATIKA MADAI MENGINE, LEMA ANAMLALAMIKIA, JAJI GABRIEL RWAKIBARILA, ALIYESIKILIZA KESI HIYO KUWA ALITOA UAMUZI WAKE KWA KUZINGATIA MANENO YA UVUMI, HUKU AKIPUUZA USHAHIDI ULIOTOLEWA MAHAKAMANI HAPO.
LEMA ANADAI KUWA JAJI ALIKOSEA WAKATI ALIPOAMUA KUWA MPIGA KURA YEYOTE ANARUHUSIWA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI HATA KAMA HAKI ZAKE ZA MSINGI HAZIJAGUSWA.

No comments:

Post a Comment