Friday, September 14, 2012

BAADA YA MAANDAMANO YA WAISLAMU KWENDA NECTA KUNUKIA................
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI IMEMSIMAMISHA KAZI NA ITAMCHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU MKUU WA IDARA YA UTAFITI, TATHMINI NA HUDUMA ZA KOMPYUTA, JOSEPH MBOWE BAADA YA UCHUNGUZI KUBAINI KUWAPO KWA DOSARI KATIKA UKOKOTOAJI WA ALAMA ZA MITIHANI YA SOMO LA ISLAMIC KNOWLEDGE KATIKA KOMPYUTA.

AIDHA, WIZARA HIYO IMEAGIZA NECTA KUKOKOTOA UPYA ALAMA ZA MITIHANI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA YA SOMO HILO WALIOFELISHWA KWA BAHATI MBAYA MWAKA HUU KUTOKANA NA DOSARI HIYO NA TAYARI MATOKEO YA ALAMA HIZO YAMETOLEWA.

 

AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI DAR ES SALAAM JANA, NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO NA UFUNDI, PHILIP MULUGO ALISEMA MEI 28, MWAKA HUU, WIZARA ILIPOKEA MALALAMIKO KUTOKA BARAZA LA WAKUU WA SHULE ZA KIISLAMU, DHIDI YA MATOKEO YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MWAKA HUU KATIKA SOMO HILO.

No comments:

Post a Comment