Monday, September 3, 2012

BAVICHA WATAKA IGP MWEMA AACHIE NGAZI.



Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/09/03/14:56:56 

BARAZA LA VIJANA LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO, CHADEMA-BAVICHA MKOA WA PWANI, LIMEMTAKA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI KUJIUZULU NAFASI AMBAYO ANAYO KUTOKANA NA JESHI HILO KUSHINDWA KULINDA WANANCHI NA MALI ZAO NA KUJIHUSISHA ZAIDI NA MASUALA YA KUUA WANANCHI WASIO NA HATIA KWA MSUKUMO WA KISIASA.

AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI HIZI, MWENYEKITI WA BARAZA LA VIJANA LA CHADEMA, BW. ELLISON KINYAHA AMESEMA KUMEKUWEPO NA ONGEZEKO LA MAUAJI YA WANANCHI KILA PANAPOFANYIKA MIKUTANO YA CHAMA CHAO KWA LENGO LA KUWATISHA WANANCHI, NA AMEELEZEA TUKIO LA HIVI KARIBUNI KABISA LA KUULIWA KWA MWANDISHI WA HABARAI WA TELEVISHENI YA CHANNEL 10, BW. DAUD MWANGOSI KUWA NI USHAHIDI WA KUSHINDWA KWA JESHI HILO.

BW. KINYAHA AMEBAINISHA KITENDO HICHO NI KIELELEZO TOSHA CHA JINSI GANI JESHI LA POLISI HALIZINGATII HAKI ZA BINADAMU, KWA AJILI KUWAFURAHISHA WANASIASA WA CHAMA TAWALA, AMBAO WAMEONESHA KUSTUSHWA NA HARAKATI YA CHAMA CHAO NA HIVYO KUAMUA KUTUMIA MBINU CHAFU KUHARIBU HARAKATI ZA KISIASA ZA CHAMA CHAO NA DEMOKRASIA KWA UJUMLA NCHINI.

MWENYEKITI HUYO WA BAVICHA MKOA WA PWANI, BW. KINYAHA AMESISITIZA HIVYO KUTOKANA NA VITENDO HIVYO VYA MAUAJI AMBAVYO VIMEKUWA VINATEKELEZWA NA JESHI LA POLISI NA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI 2008-2010 WATU 52 WALIUWA KWA SABABU MBALIMBALI AMBAZO HAZINA MASHIKO, HAKUNA BUDI KWA MKUU WA JESHI HILO KUJIUZULU NAFASI HIYO KUTOKANA NA JESHI HILO KUWA ADUI WA WANANCHI NA MALI ZAO BADALA YA KUWA MLINZI WAO, HALI INAYOAASHIRIA KUSHINDWA KWA MKUU HUYO KUDHIBITI VITENDO VINAVYOKWENDA KINYUME NA JESHI HILO KUNAKOFANYWA NA BAADHI YA ASKARI WAKE KATIKA KARNE HII YA 21.

NAYE MWENYEKITI WA BAVICHA KATA YA MLANDIZI, BW. EMMANUEL LISSU AMEELEZEA KUSHANGWAZA KWAKE NA NGUVU KUBWA AMBALO JESHI LETU LA POLISI LINAZO KATIKA KUJIHUSISHA NA MASUALA YA KISIASA AMBAPO WAPO TAYARI KUUA HATA WATU MUHIMU AMBAO WANATEKELEZA WAJIBU KAMA WAO WANAVYOTEKELEZA, NA KUSIKITISHWA KIASI CHA HAJA NA MSIBA AMBAO UMEIKUTA TASNIA YA HABARI KWA KUMPOTEZA MPIGANAJI AMBAYE AMEFIA KATIKA UWANJA WA VITA, MAREHEMU. DAUD MWANGOSI MWANDISHI WA HABARI WA TELEVISHENI YA CHANNEL 10. MUNGU AILAZE SEHEMU NJEMA PEPONI.

No comments:

Post a Comment