Saturday, August 18, 2012

WAISLAM WAVAMIA KANISA MBEZI JUU


VURUGU KUBWA ZIMEIBUKA JUZI KATIKA MBEZI JUU, WILAYA YA KINONDONI, DAR ES SALAAM BAADA YA KUNDI LA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU, KUWAVAMIA NA KUWASHAMBULIA WAUMINI WA KANISA LA SALVATION MINISTRY FOR ALL NATION (SMAN), LILILOPO ENEO HILO NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI.
INADAIWA KUWA, MALI ZILIZOHARIBIWA ZINA THAMANI YA ZAIDI YA SH. MILIONI SITA AMBAPO CHANZO CHA VURUGU HIZO NI MGOGORO ULIOANZA TANGU DESEMBA 2011.
AKIZUNGUMZA NA MAJIRA, MCHUNGAJI WA KANISA HILO FRED MWAMTEMA (48), ALIDAI UVAMIZI HUO UMEFANYIKA ZAIDI YA MARA NNE NA KUHARIBU MALI ZA KANISA KWA MADAI YA KUPIGIWA KELELE WANAPOKUWA KATIKA IBADA ZAO KARIBU NA KANISA HILO.
ALISEMA WAUMINI WA KIISLAMU WALIOFANYA VURUGU HIZO NI WALE WANAOSALI KATIKA MSIKITI WA AL MUBARAK MASJID ULIOPO JIRANI NA KANISA LAO KATIKA KATA YA NDUMBWI.
“MGOGORO HUO ULIANZA MUDA MREFU, WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WALISHAKUJA MARA KADHAA NA KUDAI WANASHINDWA KUFANYA IBADA KUTOKANA NA KELELE ZINAZOTOKA KANISA,” ALISEMA.
ALIONGEZA KUWA KUTOKAANA NA HALI HIYO, VIONGOZI WA MSIKITI HUO WALIOAMUA KUWASHTAKI KWA OFISA MTENDAJI WA KATA HIYO LAKINI HAKUNA MUAFAKA ULIOWEZA KUPATIKANA.
MCHUNGAJI MWAMTEMA ALISEMA AGOSTI 12 MWAKA HUU, WAKIWA KWENYE IBADA, GHAFLA WALIVAMIA NA KUNDI LA WAISLAMU, KUWAPIGA WAUMINI NA KUHARIBU MALI ZA KANISA KAMA VITI, VYOMBO VYA MUZIKI, MATURUBAI, KUCHOMA MOTO KAPETI NA KUNG'OA NYAYA ZA UMEME.
“TUNAOMBA VYOMBO VYA DOLA VIINGILIE KATI MGOGORO HUU ILI UWEZE KUPATIWA UFUMBUZI WA HARAKA KWANI UNAWEZA KUSABABISHA MADHARA KAMA HATUA HAZITACHUKULIWA,” ALISEMA.
ALISEMA UONGOZI WA KANISA HILO ULIAMUA KUTOA TAARIFA KITUO CHA POLISI CHA KAWE AMBAPO WAUMINI WA DINI HIZO, WALITAKIWA KUACHA KUFANYIANA FUJO NA KILA MMOJA AHESHIMU DINI YA MWENZAKE.
PAMOJA POLISI KUTOA AGIZO HILO, INADAIWA WAUMINI WA KIISLAMU WALIVAMIA TENA KANISA HILO AGOSTI 15 MWAKA HUU, WAKATI WA MKESHA NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI.
JUHUDI ZA GAZETI HILI KUWAPATA VIONGOZI WA MSIKITI HUO ZILISHINDIKANA LAKINI MUUMINI MMOJA AMBAYE HAKUTAKA JINA LAKE LIANDIKWE GAZETINI, ALISEMA WAISLAMU NDIO WALIKUWA WA KWANZA KUJENGA MSIKITI KATIKA ENEO HILO.
“BAADA YA MUDA TUKAONA WENZETU NAO WANAJENGA KANISA NA KUPIGA KELELE WAKITUMIA MATARUMBETA WAKATI WAISLAMU WAKIWA KWENYE IBADA ZAO HIVYO KUSABABISHA MGOGORO HUU KUENDELEA,” ALISEMA.
AKITHIBITISHIA KUTOKA KWA VURUGU HIZO, KAIMU KAMANDA MKOA WA KIPOLISI KINONDONI, JOHN MTALIMBO, ALISEMA MGOGORO HUO UMEDUMU MUDA MREFU BILA MUAFAKA KUPATIKANA.
“MTOA TAARIFA MCHUNGAJI MWAMTEMA AMBAYE NDIYE KIONGOZI WA KANISA HILI ALIDA WAUMINI WA KIISLAMU WANAWAFANYIA VURUGU AMBAPO KUNDI LA WATU 30 AKIWEMO SHEKHE WA MSIKITI HUU ABDU SWEDI (41), MKAZI WA MBEZI JUU, WALIVAMIA KATIKA KANISA HILO NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI,” ALISEMA.
ALISEMA KUTOKANA NA HALI HIYO, MCHUNGAJI MWINGINE WA KANISA HILI ELIA SUDI (32), MKAZI WA MWANANYAMALA, ALIJERUHIWA VIBAYA KICHWANI KWA KUPIGWA NA KITU CHENYE NCHA KALI.
KAMANDA MTALIMBO ALISEMA VURUGU HIZO ZILISABABISHA UHARIBIFU WA VITI 25 VYA PLASTIKI, VIPAZA SAUTI VINNE NA KUIBWA KWA KAMERA AINA YA SANYO AMBAPO JESHI HILO LINAMSHIKILIA SHEKHE SWEDI.

No comments:

Post a Comment