Wednesday, August 15, 2012

MUAMBA ATUNDIKA DARUGA RASMIMCHEZAJI WA KIUNGO CHA KATI WA BOLTON, FABRICE MUAMBA AMETANGAZA KUWA AMESTAAFU KAMA MCHEZAJI WA KULIPWA WA SOKA.
MUAMBA, MWENYE UMRI WA MIAKA 24, ALIZIRAI NA KUPATA MSHUTUKO WA MOYO TAREHE KUMI NA SABA MWEZI MACHI MWAKA HUU WAKATI BOLTON ILIPOKUWA IKICHUANA NA TOTTENHAM HOTSPURS.
AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI MUAMBA, ALISEMA LICHA YA HABARI HIZO KUWA ZA KUHUZUNISHA, ANAWASHUKURU MASHABIKI WAKE NA WASIMAMIZI WA KLABU HIYO.
''NAMSHUKURU MUNGU KUWA NIKO HAI HII LEO NA KWA MARA NYINGINE NAWASHUKURU SANA MADAKTARI WOTE AMBAO HAWAKUFA MOYO WAKATI NILIKUWA NA MATATIZO'' ALISEMA MUAMBA.

No comments:

Post a Comment