Friday, August 17, 2012

ECUADOR IMEKUBALI KUMPA HIFADHI YA KISIASA MWANZILISHI NA MMILIKI WA MTANDAO WA WIKILEAKS JULIAN ASSANGE.




ECUADOR IMEKUBALI KUMPA HIFADHI YA KISIASA MWANZILISHI NA MMILIKI WA MTANDAO WA WIKILEAKS JULIAN ASSANGE.
TANGAZO HILO LIMETOLEWA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ECUADOR RICARDO PATINO, KWA KILE ALICHOKIELEZA KUWA SERIKALI YAKE IMEAMUA KUMPAA HIFADHI HIYO  KUTOKANA NA WASIWASI WA HAKI ZAKE ZA KIBINADAMU KUKIUKWA.
PATINO AMEONGEZA KUWA UAMUZI HUO UMETOLEWA NA SERIKALI BAADA YA MASHAURIANO YA MUDA MREFU NA SERIKALI YA UINGEREZA NA MAREKANI KUGONGA MWAMBA.
AIDHA, ECUADOR IMEELEZA KUWA UAMUZI WAKE NI WA KULINDA HAKI ZA WANYONGE KAMA ASSANGE AMBAYE HUENDA AKAULIWA KISIASA IKIWA ATASAFIRISHWA NCHINI SWEDEN.
UAMUZI HUU WA ECUADOR HUENDA UKADHOOFISHA UHUSIANO WAKE WA KIDIPLOMASIA NA  UINGEREZA .
UINGEREZA IMESEMA KUWA HAITAKUBALI ASSANGE KUONDOKA NCHINI HUMO LICHA YA ECUADOR KUKUBALI KUMPA HIFADHI YA KISIASA, KWA KILE INACHOKISEMA KUWA INA HAKI YA KUMKAMATA .
POLISI WAMEKABILIANA NA WAANDAMANAJI WANAOMUUNGA ASSANGE NJE YA UBALOZI WA ECUADOR JIJINI LONDON NA KUWAKAMATA WAANDAMAJI WATATU.
ASSANGE RAIA WA AUSTRALIA ALIGONGA VICHWA VYA HABARI VYA KIMATAIFA BAADA YA KUTOA SIRI AMBAZO ZILIABISHA MATAIFA MAKUBWA DUNIANI KAMA MAREKANI MWAKA 2010.
JULIAN  ASSANGE ANATAKIWA NCHINI SWEDEN KWA TUHMA ZA UBAKAJI AMBAZO AMEPINGA KUHUSIKA NA KUSEMA NI ZA KISIASA NA ZINALENGA KUMWANGAMIZA.
TANGU MWEZI WA JUNI ASSANGE AMEKUWA AKIJIFICHA KATIKA UBALOZI WA ECUADOR JIJINI LONDON UINGEREZA BAADA YA UINGEREZA KUONESHA NIA YA KUMSAFIRISHA NCHINI SWEDEN KUFUNGULIWA MASHTAKA HAYO YA UBAKAJI.
SIKU YA JUMATANO ECUADOR ILISHTUMU UINGEREZA KUWA NA MPANGO WA KUVAMIA UBALOZI WAKE NA KUMKAMATA ASSANGE KWA NGUVU, TUHMA AMBAZO MTANDAO WA WIKILEAKS UNAKASHIFU .
UINGEREZA IMEKUWA IKISISITIA KUWA INA HAKI YA KUMSAFIRISHA ASSANGE NCHINI SWEDEN LAKINI ASSANGE MWENYEWE ANAONA KUWA IKIWA ATAKAMATWA NA UINGEREZA ATASAFIRISHWA MAREKANI NA KUFUNGULIWA MASHTAKA DHIDI YA UTOAJI WA SIRI ZA SERIKALI HIYO.
 

No comments:

Post a Comment