Monday, July 2, 2012

UMITASHUMTA YAANZA PWANI


BEN KOMBA/PWANI-TANZANIA/7/2/2012 1:40:12 PM

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI, BW. SHUKURU KAWAMBWA AMEWATAKA WAAMUZI WANAOCHEZESHA MICHEZO YA UMTASHUMTA KUCHEZESHA MICHEZO HIYO KWA KUFUATA MISINGI YA HAKI ILI KUINUA KIWANGO CHA MICHEZO NCHINI.

AKIFUNGUA MICHEZO YA UMITASHUMTA NGAZI YA TAIFA KATIKA VIWANJA VYA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA, BW. KAWAMBWA AMESEMA WAAMUZI WANATAKIWA KUTOA UAMUZI WA HAKI BILA UPENDELEO NA AMEWAHIMIZA KUKUMBUKA KIAPO WALICHOKILA KABLA YA MASHINDANO.

AMEAHIDI SERIKALI ITAHAKIKISHA INAYABORESHA MASHINDANO HAYO ILI KUWEZA KUFIKIA MALENGO AMBAYO IMEJIWEKEA YA KUINUA VIPAJI VYA WANAMICHEZO CHIPUKIZI AMBAO WATUTAWAKILISHA VYEMA KATIKA MICHEZO MBALIMBALI YA KIMATAIFA.

NAYE MKUU WA MKOA WA PWANI BI. MWANTUMU MAHIZA AMEISHUKURU SERIKALI KWA KUIFANYA PWANI KUWA NI KMITUO MAALUM CHA KUFANYIA MICHEZO HIYO NA KWA UPANDE WA SERIKALI YA MKOA IMEAAHIDI KUFANYIA UKARABATI VIWANJA VYA MICHEZO ILI KUSAIDIA KUWEPO KWA USHINDANI WA KWELI.

MASHINDANO HAYO YANASHIRIKISHA JUMLA YA KANDA 11, NA KUSHIRIKISHA WANAMICHEZO 1515, MICHEZO HIYO IMEANZISHWA MWAKA 1975 NA MICHEZO ITAKAYOSHINDANIWA NI MPIRA WA MIGUU, NETIBOLI, WAVU, KIKAPU NA RIADHA NA KWA UPANDE WA TAALUMA WATASHINDANISHWA KATIKA MASOMO YA SAYANSI, KIINGREZA, HATI, UBUNIFU NA HESABU.

No comments:

Post a Comment