Monday, July 2, 2012

NI HISPANIA


MFUNGAJI WA GOLI LA KWANZA

DAVID SILVA ALIIFUNGIA UHISPANIA BAO LA KWANZA, NA KABLA NUSU YA KWANZA YA MCHEZO KUMALIZIKA, MCHEZAJI MPYA WA BARCELONA, JORDI ALBA ALIANDIKISHA BAO LA PILI, BAADA YA KUKIMBIA KWA KASI NA KUMALIZIA KWA USTADI KABISA.

MFUNGAJI WA BAO LA PILI

INGAWA ITALIA WALIKUWA NA UPUNGUFU WA MCHEZAJI MMOJA, BAADA YA KUMPOTEZA MCHEZAJI WA ZAMU WA TATU THIAGO MOTTA BAADA YA KUJERUHIWA, WALICHEZA KWA BIDII, LAKINI WATAALAMU WA KANDANDA KWA UPANDE WA KUPOKEZANA MPIRA, UHISPANIA, WALIWADUNISHA KABISA.


FERNANDO TORRES ALIINGIA KAMA MCHEZAJI WA ZAMU, NA AKAFANIKIWA KUUBADILISHA MCHEZO, NA AKIANDIKISHA BAO LA TATU LA UHISPANIA,


 KABLA YA MWENZAKE KATIKA KLABU YA CHELSEA, JUAN MATA, KUANDIKISHA BAO LA NNE NA LA MWISHO LA ITALIA, NA AMBALO BILA SHAKA LILIWAVUNJA MOYO KABISA MASHABIKI WOTE WA ITALIA.

Uhispania
ITALIA ITAWEZA KUJIVUNIA NAMNA ILIFIKA KATIKA FAINALI, LICHA YA KUSHINDWA KWA MAGOLI MENGI NA TIMU AMBAYO ILIKUWA NI WAZI IMO KATIKA KIWANGO CHA PEKEE.

No comments:

Post a Comment