Tuesday, July 10, 2012

MWAKA MMOJA WA UHURU WA SUDANI KUSINI


MAELFU YA RAIA WA SUDAN KUSINI WAMEJITOKEZA BARABARANI KUSHEREHEKEA MWAKA MMOJA WA UHURU WA TAIFA LAO.
NI SHAMRA SHAMRA MJINI JUBA HUKU WATU WAKICHEZA KWA FURAHA NA KUPEPERUSHA VIJIBENDERA VYA TAIFA LAO.
NA KANDO SHEREHE RASMI AMBAZO KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BAN KI MOON ANATARAJIWA KUHUDHURIA ZINAENDELEA.
MWANDISHI WA BBC MJINI JUBA NYAMBURA WAMBUGU, ANASEMA KWAMBA WATU WENGI WANASEMA UMEKUWA MWAKA ,MZURI KWAO LICHA YA MATATATIZO KADHAA YA KIMAISHA.
HATA HIVYO MWANDISHI HUYO ANASEMA IMEKUWA NI MIEZI 12 YA MISUKOSUKO KUKIWA NA VITA VYA KIKABILA HASA KATIKA JIMBO LA JONGLE AMBAPO MAMIA YA WATU WALIWAWA . TATIZO LENGINE KATIKA KIPINDI HICHO CHA MIEZI 12 NI MAKABILIANO KATI SUDAN KUSINI NA JIRANI ZAO KHARTOUM KUHUSU MAENEO YA MIPAKA. DOA LENGINE KATIKA KIPINDI HICHO ILIKUWA NA KASHFA YA UFISADI MIONGONI MWA MAAFISA WAKUU SERIKALINI.
MBALI NA BAN KI MOON VIONGOZI KUTOKA KENYA, UGANDA NA ETHIOPIA PIA WANATARAJIWA KUHUDHURIA SHEREHE HIZO KANDO YA KABURI LA KIONGOZI WA SUNDAN KUSINI MAREHEMU JOHN GARANG.
HATA HIVYO HAKUNA KIONGOZI YEYOTE KUTOKA KHARTOUM ALITARAJIWA KUHUDHURIA.

No comments:

Post a Comment