Saturday, July 7, 2012

AHUWENI KWA WALIOFOJI VYETI JESHINI


JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ), LIMEACHANA NA UCHUNGUZI DHIDI YA KASHFA YA ASKARI 948  WALIDAIWA KUGUNDULIKA KUTUMIA VYETI VYENYE MAJINA YANAYOFANANA NA WAAJIRIWA WENGINE SERIKALINI.
JWTZ IMETHIBITISHA KUACHANA NA MPANGO HUO.
KASHFA HIYO ILIIBULIWA NA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) MWEZI MEI MWAKA HUU, AMBAYO ILIWATUHUMU ASKARI  WA JWTZ NA POLISI KUJIHUSISHA NA UDANGANYIFU HUO.
LICHA YA JWTZ KUTOA TAMKO MARA MOJA KUWA WATAFANYA UCHUNGUZI NA KUCHUKUA HATUA MUAFAKA, JANA MSEMAJI WAKE ALISEMA WAMESITISHA MCHAKATO HUO.
“HUO UCHUNGUZI HAUPO,” ALISEMA MKURUGENZI WA HABARI NA UHUSIANO WA JWTZ, KANALI KAPAMBALA MGAWE JANA.
SABABU YA KUSITISHA MCHAKATO, MGAWE ALISEMA NI BAADA YA JWTZ KUWASILIANA NA NIDA NA KUBAINI KUWA TATIZO HALIKUWA NI VYETI BANDIA BALI NI KASORO KWENYE UJAZAJI WA FOMU MAALUMU WALIZOJAZA ASKARI HAO.

No comments:

Post a Comment