Thursday, June 28, 2012

WAASI WA TUAREG WATIMULIWA GAO,MALI


 waasi nchini Mali

MAJESHI YA KIISLAM YANAYOHUSISHWA NA MTANDAO WA KIGAIDI WA AL QAEDA YAMETEKA MJI MUHIMU WA GAO, KASKAZINI MWA MALI, BAADA YA SIKU MOJA YA MAPIGANO MAKALI DHIDI YA MAHASIMU WAO WA KIKUNDI CHA TUAREG.
WATU WAPATAO ISHIRINI WAMEUAWA.
MSEMAJI WA TUAREG AMESEMA KIONGOZI WAO WA KISIASA AMEJERUHIWA KATIKA MAPIGANO HAYO SIKU YA JUMANNE, NA AMEPELEKWA NCHI JIRANI KWA MATIBABU.
WAKAZI KATIKA MJI HUO WAMESEMA KUWA WAASI WAMETEKA MAJENGO KATIKA MJI HUO NA KUPEPERUSHA BENDERA ZENYE RANGI NYEUSI.
BAADA YA WIKI KADHAA YA MAKUBALIANO YA MASHAKA KATIKA MJI WA GAO, NA BAADA YA KUSHINDWA KUUNGANA, WAPIGANAJI WA TUAREG WAMERIPOTIWA KUONDOLEWA KATIKA MJI HUO MUHIMU NA WAASI HAO WANAOTAKA KUWEKA SHERIA ZA KIISLAMU, ZA SHARIA.

No comments:

Post a Comment