Friday, June 22, 2012

VIELELEZO KESI YA LULU

MAWAKILI WA SERIKALI JANA WALIWASILISHA VIELELEZO MAHAKAMA KUU KUTHIBITISHA KWAMBA UMRI WA MSANII WA FILAMU ELIZABERT MICHAEL NI ZAIDI YA MIAKA 18.HABARI ZILIZOLIFIKIA GAZETI HILI NA KUTHIBITISHWA NA MAWAKILI WAWILI; MMOJA WA LULU NA MWINGINE WA SERIKALI AMBAO HAWAKUTAKA KUTAJWA, ZIMEELEZA KUWA VIELELEZO HIVYO VIMEWASILISHWA JANA MAHAKAMANI HAPO.

HABARI ZIMEELEZA KUWA MOJA YA VIELELEZO HIVYO VYA JAMHURI NI MKANDA WA VIDEO AINA YA CD, YENYE MAHOHJIANO KATI YA MSHTAKIWA HUYO NA MTANGAZAJI MMOJA NCHINI.
"VINGINE NI MAELEZO YA MSHTAKIWA HUYO ALIYOYATOA POLISI WAKATI ALIPOHOJIWA KUHUSU TUHUMA ZINAZOMKABILI, MAOMBI YA HATI YA KUSAFIRIA (PASSPORT) NA MAOMBI YA LESENI YA UDEREVA, ALISEMA MMOJA WA MAWAKILI HAO.No comments:

Post a Comment