Friday, June 29, 2012

RAAWU: SERIKALI INAHUSIKA KUTEKWA DK ULIMBOKA


CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA ELIMU YA JUU, SAYANSI, TEKNOLOJIA, HABARI NA UTAFITI NCHINI (RAAWU), KANDA YA ZIWA KIMELAANI VIKALI KITENDO CHA KINYAMA CHA KUPIGWA NA KUUMIZWA VIBAYA, ALICHOFANYIWA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA, DK. STEVEN ULIMBOKA, NA KUDAI KWAMBA, UNYAMA HUO UMEFANYWA NA SERIKALI YENYEWE.
KATIBU WA RAAWU KANDA YA ZIWA, RAMADHANI MWENDWA, AKISISITIZA JAMBO HUKU AKIONESHA VITABU VYA SHERIA NA UTUMISHI. (PICHA NA SITTA TUMMA).
RAAWU IMESEMA, USHAHIDI WA MAZINGIRA UNAONESHA DHAHIRI SHAHIRI KWAMBA SERIKALI IMEHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KUMDHURU KIONGOZI HUYO WA MADAKTARI NCHINI, IKIWA NI LENGO LA KUTAKA KUZIMA MGOMO WA MADAKTARI UNAOENDELEA KATIKA KUDAI MASLAHI NA HUDUMA BORA YA MATIBABU KWA WATANZANIA.
KAULI HIYO IMETOLEWA MCHANA WA LEO JIJINI MWANZA NA KATIBU WA RAAWU KANDA YA ZIWA, RAMADHANI MWENDWA, WAKATI ALIPOZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI HIZI OFISINI KWAKE KUHUSIANA NA TUKIO HILO LA KINYAMA, LILILOTOKEA MAJIRA YA SAA 6 USIKU WA KUMKIA JUZI, AMBAPO WATU WATATU WANAODAIWA KUWA NA SILAHA AINA YA SHORT GUN NA BASTOLA WALIMTEKA DK. ULIMBOKA ENEO LA BARABARA YA TUNISIA, KINONDONI JIJINI DA RE SALAAM.
“RAAWU TUNALAANI VIKALI SANA UNYAMA HUU. NA HAPA MIMI NINADHANI SERIKALI IMEHUSIKA KUMDHURU KIONGOZI HUYU WA MADAKTARI NCHINI. HUU NI UNYAMA USIOVUMILIKA WALA KUFUMBIWA MACHO.
“SERIKALI BADALA YA KUTATUA MATATIZO INAANZA KUTUMIA MABAVU KUWAPIGA VIONGOZI WANAOTETEA MASLAHI YA WATANZANIA. ISIJIDANGANYE KWAMBA KUTUMIA MABAVU NDIYO ITAKUWA SULUHU YA MATATIZO. KWA UNYAMA ALIOFANYIWA DK. ULIMBOKA IWE CHEMICHEMI YA WAFANYAKAZI WOTE KUUNGANA NA VIONGOZI WAO KUDAI KWA NGUVU ZOTE HAKI ZAO”, ALISEMA KATIBU MWENDWA.

No comments:

Post a Comment