Monday, June 11, 2012

MSAFARA WA VIONGOZI WA UINGEREZA WASHAMBULIWA


MSAFARA WA MAGARI ULIOKUWA UMEBEBA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI LIBYA UMESHAMBULIWA MJINI BENGHAZI MJI WA PILI KWA UKUBWA NCHINI HUMO.
MSEMAJI WA UBALOZI, AMETAJA SHAMBULIO HILO KAMA BAYA SANA NA KUELEZEA KUWA MAAFISA WAWILI WA ULINZI WAMEJERUHIWA.
RIPOTI ZINASEMA KUWA MSAFARA HUO ULISHAMBULIWA KWA ROKETI WAKATI ILIPOKUWA INAPITA KARIBU NA OFISI YA UBALOZI.
HIVI KARIBUNI KUMEKUWA NA MASHAMBULIZI DHIDI YA MASILAHI YA KIGENI YA NCHI ZA KIGENI NCHINI LIBYA, HUKU WIKI JANA TU SHAMBULIO LILIFANYWA KARIBU NA OFISI YA UBALOZI WA MAREKANI.

No comments:

Post a Comment